Kwenye dunia ya 5G unaweza kusema Oppo wanasogea kwa kasi kwa sababu ni kampuni ambayo haina miaka mingi kwenye biashara hii ya simu janja lakini tayari ulimwengu unaijua bila kusahau simu janja kama Oppo Reno6 Pro 5G.
Katika mwendelezo wa kuzichambua simu tatu ambazo zimezinduliwa hivi karibuni leo hii pata nafasi ya kufahamu undani wa Oppo Reno6 Pro 5G ambayo ina mengi kuliko toleo la nyuma yake. Je, unajiuliza simu hii ina sifa gani? Fuatana nami mpaka mwisho wa makala hii.
Kioo :
- Ukubwa: Urefu wa inchi 6.55
- Ubora: AMOLED (1080*2400px, 90Hz); ina ung’avu wa hali ya juu sana kufanya kinachoonekana kivutie
Memori :
- Diski uhifadhi: 128GB/256GB
- RAM: GB 8 na 12
Kamera :
- Kamera Kuu: MP 64, 8, 2 na 2+taa moja ya kuongeza mwangaza sehemu ambazo kuna mwanga hafifu. Ina uwezo wa kurekodi picha mnato za ubora wa 4K na 1080px
- Kamera ya Mbele: MP 32+uwezo wa kurekodi picha mnato za ubora wa 1080px
Oppo Reno6 Pro 5G: Muonekano wa nyuma na mpangilio wa kamera. Upande wa mbele unalindwa na Corning Gorilla Glass 5, nyuma-kioo.
Betri/Chaji :
- Li-Ion 4500 mAh
- USB-C 3.1, OTG+uwezo wa kuchaji haraka kwa nguvu ya 65W, inatumia “Super VOOC 2.0” ambayo inafanya chaji kujaa haraka
Kipuri mama :
- MediaTek Dimensity 1200 5G
Uzito :
- Gramu 177
Programu Endeshi
- ColorOS 11.3, Android 11
Rangi/Bei :
- Nyeusi na Bluu
- Bei yake inaanzia $530 (zaidi ya Tsh. 1,219,000) kwa bei ya ughaibuni
Simu hii haina sehemu ya kuchomeka spika za masikioni, memori ya ziada, inatumia kadi mbili za simu, teknolojia ya kutumia alama ya kidole ipo kwa pembeni, mnara wa mawasiliano ni GSM / CDMA / HSPA / CDMA2000 / LTE / 5G, Bluetooth 5.2, WiFi.
Kwa yeyote ambae anapenda simu yenye uwezo mkubwa rununu hii inaweza kuwa ni chaguo zuri kutokana na yale ambayo yanapatikana humo. Tunakaribisha maoni yako.
Vyanzo: Gadgets 360, mitandao mbalimbali
No Comment! Be the first one.