Labda tatizo sio simu kwamba ni kubwa ila nguo yako ya ‘kubana’. Utakuta mtu kavaa suruali ya kushika mwili (kubana) na hawezi kabisa weka simu mfukoni anabaki kuishikilia tuu. Sasa baadhi ya watumiaji wa iPhone 6 Plus wamepata ufumbuzi ni vipi wataweza beba simu zao mifukoni mwa suruali.
“Nilijaribu kutoa simu mfukoni, Nikaitoa kwa shida bado kidogo nigongwe na gari!. Tumefanya hivi ili iwe rahisi kufikia simu yako ukiwa umesimama hata ukiwa umekaa” alisema CEO wa I/ODENIM
Kampuni ya Innovative Obsession Denim (IODENIM) ambayo inatengeneza nguo, imekuja na mali mpya ya jeans ambazo zina mifuko spesheli kwa ajili ya kuwekea simu. Mifuko hii iko kwa iPhone 6 Plus licha ya kwamba hata simu-janja zingine kama Samsung Gallaxy s5 nayo inaweza kaa bila matatizo. Kampuni hiyo imetengeneza mifuko hiyo ya jeans karibia isionekane (imejificha kidogo) lakini ni rahisi kutoa na kuweka simu mfukoni kwa sababu mfuko wake uko pembeni mwa paja (sio mbele wala nyuma) mifuko hi imepewa jina la I/O Pockets
Hapo mwanzo mifuko hii ilikua kwa ajili ya smartphones ndogo ndogo lakini imeongezwa ukubwa kwa kua na simu nazo zimeongezwa ukubwa. Nguo nyingine kama Carhartts na Kuhls, zina mifuko mikubwa ila wateja wanalalamika wanasema simu zao hazika ‘tuli’ mifukoni.
FAIDA: kwa kutumia suruali hizi hupati shida na pia simu haipati misukosuko mingi kama ingekua mbele au nyuma ya mfuko sababu simu hii inakaa pembeni mwa mguu, Pia haikuchori na sio rahisi mtu kujua kama umebeba simu… hata wale ‘wakwapuaji’ watasubiri.
Tuambie je wewe utanunua nguo hizi zikija nchini?
Soma kuhusu iPhone 6 na iPhone Plus HAPA.
No Comment! Be the first one.