fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Android apps iOS Reels

Uwezo wa kusambaza na kutunza picha jongefu kwenye Reels

Spread the love

Katika ulimwengu wa vile picha za mnato ambazo ni fupifupi ndani ya Instagram unaweza kuzifyatua kupitia Reels ambayo imekuwa mshindani wa karibu kwa TikTok.

Reels” ni nini?

Hiki ni kipengele kinachopatikana ndani ya Instagram (upande wa kushoto juu-kwenye alama ya kamera) ambapo inamuwezesha mtu kuweza kuchapicha picha ama picha mnato yenye urefu wa kati ya sekunde 15 mpaka  sekunde thelathini (30).

kutunza picha

Namna ya kufikia kipengele cha Reels ndani ya Instagram.

Reels ndani ya Instagram imekuwa ikiendelea kupata umaarufu kutokana na urahisi wa kuitumia hasa ukizingatia imewekwa ndani ya programu tumishi mama hivyo kuifanya kuwa moja ya vipengele ndani ya Instagram. Kwa miezi ya karibuni Reels imekuwa ikifanyiwa maboresho na kwa mujibu wa masasisho ya hivi karibuni mtumiaji anaweza kuhifadhi lakini pia kusambaza chapisho lililowekwa huko.

Maboresho hayo yanamuwezesha mtumiaji kuwa na uwenzo wa kutunza vhapisho ambalo limemvutia kwa ajili ya matumizi ya baadae au hata kulisambaza kwa wengine kupitia jumbe za moja kwa moja (Direct messages) ili nao waweze kulitazama. Vilevile, unaweza ukachagua mdundo ambao utapenda uende sambaba na chapisho la picha/picha mnato hivyo kufanya mtu atayekuwa ana angalia kuweza kuona na kusikia sauti nya wimbo/mdundo utakaokuwa umeuchagua kutoka kwenye orodha ndani ya kipengele husika.

kutunza picha

Sasa mtu anaweza kutunza picha na kusambaza chapisho kutoka wenye Reels.

Kama wewe ni mtuaji wa Reels ndani ya Instagram pengine habari hii ya kuweza kutunza picha au kusambaza itakuwa imekuvutia. Tungependa kusikia maoni yako na kumbuka kutembelea tovuti ya TeknoKona kila siku kwa habari mbalimbali zinazohusu teknolojia.

Chanzo: Gadgets 360

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania