Makamu raisi wa uinjinia kutoka Android bwana Dave Burke anasema toleo la majaribio la Android 12 ndio toleo la majaribio (beta) kutoka Android ambalo limeshushwa sana kuliko mengine yote.
Japokua hajataja namba kamili ya idadi ya mashusho hayo, kwa upande mwingine amesema kuwa toleo hili litakua na mapokezi ya aina yake kwani wengi wana shauku ya kuwa nalo kwa hali inavyoonyesha.

Soma Kila Kitu Kuhusu Android 12 —> Hapa <—
Namba hii ya ukubwa wa kushushwa inaelekea imetokana na maboresho yaliyofanyika katika os hii, maboresho hayo ni pamoja na yale ya kimuonekano na maboresho ya sera nzima ya faragha.
Android 12's beta is by far our most downloaded/installed beta ever. Speaking of which, Beta 2 is available today: https://t.co/VR8CtXKWkZ
— Dave Burke (@davey_burke) June 9, 2021
Toleo hilo la majaribio linapatikana katika baadhi ya simu za Google pixel, OnePlus, Xiaomi, OPPO, Realme, Nokia, Vivo, ASUS, Tecno, Sharp, TCL, na ZTE huku Samsung wao wakilazimika kusubiria ili kuanza kutumia toleo hilo la beta
No Comment! Be the first one.