IMEI namba ni kitu muhimu sana wakati pale simu janja yako imeibiwa au umepoteza na unataka kufanya jitihada za kuipata tena. Kwa polisi ni lazima utapeleka na taarifa IMEI ya simu husika. Vilevile, kama una mpango wa kui’track simu hiyo ndio njia mojawapo.
Ni wazi kwamba inajulikana ukiwa na kifaa chako unaweza ukapata IMEI ya simu yako baada ya kupiga *#06# katika simu yako. Ssasa kama hilo linawezekana hivyo vipi ukiibiwa kifaa chako hicho?
IMEI kwa kirefu chake ni ‘International Mobile Equipment Identity‘ ambapo kwa haraka haraka ni namba ambazo zinakuwa kama utambulisho wa kifaa na katika simu, mara nyingi zinakuwa tarakimu15. Namba hizi huwa hazifanani na zinakuwa katika kifaa kimoja tu.
Faida yake inakuja pale unapokuwa umepoteza kifaa chako kwa sababu namba hiyo ni moja tu kwa kifaa kile hivyo itakuwezesha kuweza kufuatilia nyendo za simu hiyo kama ikiwa imeunganishwa na intaneti.
Ukiachana na kuipata simu janja hiyo. Vilevile, unaweza ukaamua kufuta kila kitu na kuifunga kabisa simu hiyo kutoweza tumika tena kupitia IMEI ya simu hiyo.
JINSI YA KUPATA IMEI YAKO KAMA HUNA KIFAA CHAKO
Kama huna simu janja yako karibu na wewe unaweza ukapata IMEI kwa kutumia Find my device kwa wale wa Android na Find My Phone kwa wale wanaotumia vifaa vya Apple.
Android.
Kwa watumiaji wa Android ni kwamba unaweza kupata IMEI yako kwa kutumia akaunti ya Google ambayo ulikua umeiweka katika simu yako (uliyokuwa unatumia katika PlayStore).
- Kwa kuingia katika Android Device Manager kupitia kompyuta
- Ingia kupitia akaunti yako ya Google ambayo ulikua unaitumia katika simu yako.
- Ukifanikiwa kuingia humo utaona vifaa vyote ambavyo vimeungwa na akaunti hiyo, unaweza chagua kifaa husika na kuone taarifa zake ikiwemo IMEI.
Apple.
Kwa kutumia kompyuta yako ingia katika tovuti ya Apple
- Ingia katika Akaunti yako kwa kutumia Apple ID
- Ukishaingia nenda katika orodha ya vifaa kisha chagua jina la kifaa
- Taarifa za kifaa husika zitatokea ikiwemo na IMEI ya kifaa hicho.
Hizi ndio njia ambazo zinafanya kazi katika simu zote za Android na iPhone. Hivyo basi naamini zile kesi za kuacha kufuatilia kifaa chako kisa umesahau IMEI hazitakuwepo tena.
Kuna wengine wanahofia kwenda Polisi kutoa ripoti ya kuibiwa simu zao kisa wataulizwa IMEI za vifaa vyao na wao hawana hifadhi/kumbukumbu ya namba hizo.
Tembelea TeknoKona Kila Siku Kujipatia Maujanja Kedekede Ya Teknolojia. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.