fbpx

Kivinjari cha Microsoft Edge kupatikana katika Android na iOS

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Kampuni ya Microsoft imetangaza kwamba kivinjari/kisakuzi (Browser) chake cha Microsoft Edge sasa kitapatikana katika mifumo ya Simu Janja za Android na iOS.

Microsoft Edge imekuwa ikitumika kama kivinjari katika mfumo wa Kompyuta wa Windows 10 na imekuwa na maboresho mazuri zaidi kuliko Internet Explorer.

Microsoft Edge ni mrithi wa Internet Explorer iliyokuwa ikitumika katika mfumo endeshi wa Windows kwa kipindi chote cha nyuma.

Microsoft Edge kupatikana katika Android

Kivinjari cha Microsoft Edge kupatikana katika Android na iOS

Microsoft imethibitisha Edge itapatikana katika mifumo ya Android na iOS na kwa sasa kuna toleo la Beta ambapo kufikia mpaka mwishoni mwa mwaka watakuwa wametoa toleo kamili kwa wote.

INAYOHUSIANA  M-Paper: App ya Tanzania Inayokupatia Magazeti Mbalimbali Kwenye Simu/Tableti Yako

Kuwepo kwa Edge katika mifumo ya Simu Janja kutaongeza upinzani na vita kali kwa vivinjari maarufu vya Safari ya Apple, Chrome ya Google, Firefox ya Mozilla, Opera na kivinjari cha Samsung.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.