fbpx

Arrow Launcher sasa kujulikana kwa jina la Microsoft Launcher

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +

ICT CONFERENCE 2019

Sambaza

Arrow Launcher sasa itafahamika kwa jina la Microsoft Launcher, Kampuni ya Microsoft imetangaza kubadili jina.

Arrow inayozalishwa na Microsoft ilianza kutumika tangu mwaka 2015 katika Simu Janja za Android na imekuwa na watumiaji wengi sehemu kadhaa za Dunia.

Launcher ni app mojawapo katika simu za mfumo wa Android ambapo kazi yake ni kubadilisha muonekano wa simu na mpangalio wa Icon pia.

Microsoft Launcher

Microsoft Launcher

Launcher zipo za aina tofauti na nyingi zinapatikana bure kupitia Play Store. Uwekaji Launcher kwa watumiaji wa Android ni jambo linalopendwa sana na wengi kwa kuwa huifanya Simu kuwa na muonekano wa kipekee na wenye kuvutia.

INAYOHUSIANA  Maboresho: WhatsApp kuleta Albamu na meseji za kufutika.

Microsoft Launcher imekuja na mabadiliko mengi kuanzia kupata habari, kalenda, Themes, Icon na mpangilio utakao mpa fursa zaidi mtumiaji kufanya anachotaka.

Microsoft Launcher pia itawawezesha watumiaji wa Android kutazama picha, kuhariri nyaraka, au kupruzi tovuti kutoka simu hadi kwenye Kompyuta zao.

Kwa sasa inapatikana Play Store kwa toleo la beta. Kwa atakayenda kujaribu na kutumia tumekuwekea link yake hapo chini.

Kwa watumiaji wa Arrow launcher watapata Maboresho hayo moja kwa moja.

Microsoft Launcher(Preview)

Facebook Comments

Sambaza

ICT CONFERENCE 2019

Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.