fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
apps Samsung

Safety Screen: App Ya Samsung Ambayo Itawafanya Watoto Kukaa Mbali Na Kioo Cha Kifaa!

Safety Screen: App Ya Samsung Ambayo Itawafanya Watoto Kukaa Mbali Na Kioo Cha Kifaa!

Spread the love

Kukaa karibu vifaa vyetu vya kielektroniki wakati tunaangalia vitu kama vile kutoka kwenye Tv ni hatari. Kumbuka hata wewe ulivyokuwa mdogo nna imani ulikua ukikatazwa kusogelea TV. Sasa basi Samsung wameliona hilo na kuja na ufumbuzi.

Sawa pengine labda kwa sasa inaweza ikawa ni vigumu kutazama Tv, najua watu wengi siku hizi wanakomaa kwenye simu na kompyuta kumbuka hata vioo hivyo vina mazara tuu pale unapo vikaribia.

Simu zetu watoto au wadogo zetu wanaweza wakawa wanazitumia kama vifaa vya kusababisha furaha yao, wanaweza wakaamua kucheza michezo mbali mbali na mda mwingine wanaweza wakatumia kama njia ya kusomea. Sasa utawezaje kuwaweka mbali na kioo cha kifaa wanachotumia

Safety Screen

Safety Screen

Shukrani kwa Samsung ambao wamekuja na App inayojulikana kama Safety Screen, hii inatumia teknolojia ya kugundua sura (facial recognition). App hii itagundua kama mtumiaji wa kifaa hicho yuko karibu na kioo cha kifaa.

Kama mtumiaji akiwa karibu na kioo basi kitatokea kikatuni, ambacho kitamjulisha mtumiaji kwamba yupo karibu na kioo cha kifaa na hivyo inabidi arudi nyuma. Endapo mtumiaji atakapoungeza umbali wa kutoka alipo na kifaa hicho basi hicho kikatuni kitaondoka, kumjulisha kwamba yupo umbali sahihi.

SOMA PIA  Simu ya Samsung Galaxy Star Pro - Simu janja ndogo, kwa bajeti ndogo

Samsung wametengeza App hii wakiwa na madhumuni mengi. Zuri kati ya madhuni hayo ni kwamba App hii itamjenga mtoto kujua njia nzuri ya umbali wa kutumia pale anapotumia vitu vya kielektroniki kama vile Tv.

App Ya Safety Screen

App Ya Safety Screen

Kumbuka kama mtu akiwa anatumia muda mwingi sana katika kuangalia kitu katika skrini ana hati hati ya kuharibu macho yake na hiyo ikiwemo kuharibu uwezo wake wa kuona kabisa.

Cha kufanya ni kupakua App hii katika kifaa chako na kuanza kuitumia. Utumiaji ni wa aina yake kwani mwenye kifaa anaweza kuiwasha na pia kulinda uwashaji huo na nenosiri. Yaani inamaanisha kama App hiyo ikiwashwa hakuna mtu anaeweza kuizima labda awe ni Yule mwenye nenosiri.

SOMA PIA  Slack imeboresha kitu na kuzidi kuvutia

Tovuti Yao ni www.samsungsafetyscreen.com
Shusha App Hiyo Hapa – Android

Niandikie sehemu ya comment hapo chini je, wewe ni mmoja kati ya wale wanaosogelea sana vifaa vyao? Na pia unahisi ukiwa na App hii itakusaidia. TeknoKona ndio gwiji la habari za kiteknolojia Tanzania kwa ujumla, tembele kila siku ujipatie mambo. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania