fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Mtandao wa Kijamii whatsapp

Groups za WhatsApp kusajiliwa huko India, Maadmin hatiani Kufungwa

Groups za WhatsApp kusajiliwa huko India, Maadmin hatiani Kufungwa

Spread the love

Serikali ya wilaya moja nchini India, Kupwara, imetambulisha utaratibu mgumu kweli kweli kwa watumiaji wa WhatsApp katika eneo lao. Utaratibu huo utawabana ma’admin wa groups pale kosa linapotendwa katika makundi waliyoyaanzisha.

Pia wafanyakazi wa serikali wameambiwa wasijihusishe na ma’group ya habari na kwamba mfanyakazi wa serikali akigundulika anashiriki katika kuongelea sera za serikali katika magroup ya WhatsApp basi hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

Kama kundi likikutwa linasambaza habari za uongo basi watu watakaochukuliwa hatua ni pamoja na ma’admin wanaoruhusu habari hizo zisambae kwenye makundi yao. Sheria hii inalenga kupunguza usambaaji wa taarifa zisizo za ukweli.

 WhatsApp kusajiliwa huko India

Makundi yote ya WhatsApp yanatakiwa kuhakikisha yamejiandikisha kwa mkuu wa wilaya hiyo. Na moja ya hatua inayochukuliwa katika uandikishaji huo inaonekana ni kuingiza namba ya chombo cha usalama katika magroup hayo ili kurahisisha ufuatiliaji wa mazungumzo.

Je una maoni gani juu hili? Ni jambo zuri au baya? Tayari watu wengi wanalipinga wakisema uongozi wa eneo la Kupwara huko India umepitiliza mipaka.

Vyanzo: hindustantimes.com na vyanzo vingine

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania