fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Apple Teknolojia Windows

Ondoa programu ya QuickTime kwenye kompyuta yako! #Usalama

Ondoa programu ya QuickTime kwenye kompyuta yako! #Usalama

Spread the love

Kama umepakua programu ya QuickTime kutoka Apple kwenye kompyuta yako ya Windows unashauriwa kuiondoa mara moja.

Watafiti mbalimbali wa mambo ya kiusalama wa kimtandao wamegundua ni rahisi sana programu hiyo kutumika kuvamia data za kompyuta zako kwa sasa.

programu ya quicktime

Tayari Apple walishatangaza kuacha kutoa masasisho (updates) kwa programu yao hiyo ambayo mara nyingi ilikuwa inakuja moja kwa moja pale unapotaka kupakua programu ya iTunes.

SOMA PIA  SN10 - SpaceX wafanikiwa kutua roketi ndege yao ya Starship kwa mara ya kwanza

Ingawa programu ya QuickTime bado inaendelea kuwa na uwezo wa kufanya kazi ila ina ubovu wa kiusalama (security vulnerabilities) ambao ni hatari kwa data zilizokwenye kompyuta yako.

Kama una programu hiyo fuata hatua hizi kuiondoa kwenye kompyuta yako;

Kwa watumiaji wa Windows 10:

  • Bofya ‘Start’.
  • Chagua “Settings.”
  • Chagua “System” na nenda eneo la “Apps and features.”
  • Tafuta QuickTime kwenye orodha na kisha bofya “Uninstall.”
SOMA PIA  Saa ya kisasa isiyochajia na kitu chochote bali na joto la mwili wa binadamu

Kwa watumiaji wa Windows 7:

  • Bofya ‘Start’.
  • Chagua “Control Panel.”
  • Chagua “Programs”  na kisha chagua na kubofya “Programs and features.”
  • Tafuta QuickTime kwenye orodha na kisha bofya “Uninstall.”

Inasemekana kwa sasa ni kwa kompyuta za Windows tuu, Apple wanaendelea kutoa masasisho ya programu hiyo kwa wale wanaotumia kwenye vifaa vyao kama vile kompyuta za Mac.

SOMA PIA  Google kufanya masasisho ya kwenye apps zake kuongeza usalama

Ni muhimu kuhakikisha unakuwa na programu zinazopata masasisho (updates) mara kwa mara ili kuzidi kukuhakikishia usalama wa data zako. Endelea kutembelea TeknoKona

vyanzo: grahamcluley.com na mitandao mbalimbali

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania