Huwezi ukataja mageuzi kumi ya teknolojia mwaka huu bila ya kutaja Chaja za wireless, ukweli ni kwamba haya ndiyo mageuzi ya pekee ambayo yamegusa watengenezaji wengi tofauti tofauti wa vifaa pia teknolojia hii imegusa aina nyingi za vifaa kutoka saa janja simu janja hadi vifaa vya viwandani kama magari.
Mafanikio ya teknolojia hii ya chaja za wireless inakuja kutokana na ukweli kwamba ni rahisi mno kuitumia, ni rahisi kuweka simu yako juu ya chaja na kuondoka bila ya kushughurika na waya wala kuchomeka lakini urahisi huu unawezesha teknolojia hii kuwa na matumizi makubwa zaidi mfano barabarani magari yanayotumia umeme yanaweza kuchajiwa katika mataa ama katika sehemu za maegesho.
Teknolojia hii kimsingi inachukua teknolojia inayotumiwa na transforma ambapo kwenye chaja yenyewe kuna kuwa na koili ambazo pindi zinapo pitishiwa umeme hutengeneza nguvu za usumaku ambazo hutumiwa na koili zilizo katika kifaa chako kutengeneza umeme tena ambao hutumika kuchaji betri ya simu ama gari ama kifaa chochote husika.
Pamoja na kuwa ni rahisi kutumia teknolojia hii ya kuchaji vifaa mbalimbali lakini pia teknolojia hii inatumika zaidi kuchaji vifaa vya baiolojia kama moyo wa bandia kwa kuvichaji kwake ni njia salama mfano haihusishi kuingiza waya ndani ya mwili, njia hii pia inasemwa kwamba ni njia ambayo inadumu muda murefu bila kuchakaa hii ni kwasababu hakuna kuchomeka chomoa kama njia nyingine (watumiaji wa chaja za simu za iPhone watakubaliana na mimi jinsi chaja zetu zinavyochakaa).
Chenye mazuri huwa hakikosi kasoro! Teknolojia hii pamoja na mazuri yake ukweli ni kwamba teknolojia hii inatumia muda mrefu zaidi kuchaji kulinganisha na njia ya kawaida, hii inasababisha watengenezaji wengi washauri kwamba watumiaji wa chaja hizi kuchaji kwa mara ya kwanza kwa njia ya kawaida. Pia teknolojia hii ya kuchaji kwa wireless inagharama kubwa kutengenezwa ukiringanisha na chaja za kawaida.
Kama ilivyo kwa kila teknolojia inakuwa na muungano wa wadau wa teknolojia husika ambao unatengeneza viwango ambavyo ndio huongoza utengenezaji wa vifaa vinavyotumiwa na teknolojia hiyo basi teknolojia hii ya chaja za wireless inatawaliwa na miungano miwili mmoja ni ule wa Wireless Power Consortium ambao unaungwa mkono na watengenezaji wa simu kama Nexus LG Microsoft na HTC na muungano mwingine ni ule wa Power Matters Alliance ambao wao wanaungwa mkono na kampuni la simu za mkononi ya AT&T ya nchini Marekani
No Comment! Be the first one.