Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
apps, Mtandao wa Kijamii, Teknolojia

Engage: App maalum kutoka Twitter kwa ajili ya mastaa

engage-app-maalum-kutoka-twitter-kwaajili-ya-ma-staa

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

Twitter imeendelea na jitihada zake za kubaki katika chat za mitandao ya kijamii duniani baada ya leo kuleta app ya Engage ambayo ni maalumu kwa ajiri ya mastaa na watu maarufu na makampuni ambayo(ambao) wana akaunti katika mtandao huu.

Engage.0.0
Muonekano mpya wa toleo la kwanza la app ya Engage

Engage ambayo ni kama app ya Twitter ya kawaida tuu isipokuwa muundo wake mzima umejikita katika kuboresha mawasiliano kati ya mtumiaji ama kampuni na wafuasi ama mashabiki  wake.

Engage inamsaidia mtumiaji kuona kwa kiasi gani mabandiko yake ama tweets zinakubalika na kwa namna ambavyo zinawagusa watu, kufuatilia mabandiko ni muhimu kwa watu maarufu na akaunti za biashara ama akaunti za makampuni kwa kuwa huwasaidia kujua kama wamefikia kiasi gani cha watu.

INAYOHUSIANA  ByteDance, wamiliki wa TikTok wasema bado watabaki na teknolojia muhimu

App hii imeanza kupatikana katika soko la app la vifaa vya iOS pengine baadae itapatikana kwa vifaa vya android pia.

Kwasasa app hii inakuja na kurasa tatu muhimu kama ifuatavyo:-

>Engage

EngageInPhone

Ukurasa huu kama ambavyo Highlights ipo katika app ya kawaida ya twitter ni kwaajiri ya kuleta habari za watu ambao wanafuatwa na wengi ya watu ambao unawafuata, pia inakuletea habari za watu unaowafuata na ambao wamekuwa verified lakini pia sehemu hiii inaleta taarifa za watu ambao unawasiliana nao zaidi.

INAYOHUSIANA  WhatsApp ya Android Yapata 'Update': Fahamu Mambo 5 Yaliyoboreshwa

>Understand

UnderstandInPhone

Ukurasa huu utakuletea takwimu za Tweets zako ambazo umekuwa ukizipost kwa mfano ni watu wangapi wame retweet ama wangapi wamezilike na pia ni watu wangapi umewafikia.

>Posts

Katika ukurasa huu utapata taarifa za kila post ambayo umeipost, je iliwafikia wangapi na taarifa kama hizo kwa kila post.

Kimsingi app hii itawasaidia mastaa, makampuni na taasisi mbali mbali ambazo zina akaunti za twitter kufikia watu wengi zaidi.

INAYOHUSIANA  Google Kuhamasisha Utumiaji Wa Umeme wa Jua

Hii ni moja kati ya hatua ambazo Twitter imekuwa inajaribu kufanya ili kukuza watumiaji hai wa mtandao huu.

Makala hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyowekwa katika blog ya Twitter

Soma zaidi: Kwanini hisa za Twitter zinazidi kuanguka sokoni

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Nickson