fbpx

Huawei yajigamba na Kirin 980

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Katika kongamano la IFA 2018 kampuni mbalimbali zimeonyesha vitu vyao vipya; Huawei wamethubutu kujigamba na Kirin 980 ambacho ni kipuri kipya kinachotegemewa kuwepo kwenye toleo lijalo la simu rununu kutoka kwao.

Kwa mujibu wa waandishi mbalimbali waliopata fursa ya kuhudhuria uzinduzi wa Kirin 980 kulingana na maelezo yaliyotolewa na wahusika, kifaa hicho kimelinganishwa ubora na Snapdragon 845 kwenye vipengele karibu vyote muhimu:

Ufanisi. Huawei wanadai kipuri hicho ni bora kwa 22% zaidi ya Snapdragon 845 kwa maana ya kwamba kasi ya kufungua programu tumishi. Upande wa kufurahia wakati wa kucheza magemu kifaa hicho kinaelezwa kuwa na utendaji mzuri wa kazi wa asilimia 22 lakini kutumia kiasi kidogo kwa maana ya32% chini zaidi kulinganisha na mpizani wake.

INAYOHUSIANA  Apple Na Samsung Watupwa Mbali: Huawei Imeongoza Mauzo China Katika Robo Ya Pili Ya 2016!

Usalama kwa kutumia teknolojia ya “Akili ya kufikirika”. Hapa Huawei wameweka nguvu kwa kuongeza vipuri vidogo viwili ndani ya Kirin 980 ambapo kazi zao ni kusaidia kuweza kutambua uso wa mtu; picha 4,500 kwa dakika.

yajigamba na Kirin 980

Kwenye teknolojia ya utashi wa kufikirika kifaa hicho kinaelezwa kutoa majibu yaliyo sahihi na kuweza kujua ni wakati gani simu intatakiwa kutumia nguvu zaidi na kuweza kupunguza pale ambapo inahitajika nguvu ndogo kufanikisha kitu fulani.

Picha. Kipuri kipya cha Kirin 980 inafanya kazi kwa 46% haraka zaidi kulinganisha na watangulizi wake huku ikiwa imeboreshwa kwa 23% kuhusu matumizi ya chaji kwa kipengele hicho pekee.

INAYOHUSIANA  Fahamu Simu za Zuri: Uchambuzi wa simu za Zuri C41 na Zuri C52

Kasi ya intaneti. Kipuri hicho ktakuwa na uwezo wa kutoa intaneti yenye kasi ya 1,732Mbps kwa njia ya Wi-Fi kwenye simu ukilinganisha na 866Mbps ambayo ipo kwenye Snapdragon 845.

Ndani ya Kirin 980 kuna jumla ya vipuri 8; viwili vikiwa na kazi ya kuongeza kasi ya ufanyaji kazi, vingine viwili kazi zao ni kuwezesha kufanya kazi kwa muda mrefu na vinne vilivyobaki jukumu lao kufanya ufanisi uwe wa juu pale ambapo hakuna kazi nyingi.

yajigamba na Kirin 980

 Ukubwa wa kipuri mama cha Kirin 980.

Kiujumla Kirin 980 ina 40% chini ukiangazia kiasi cha nguvu inachotumia na kasi yake kuwa bora zaidi kwa 20%. Kifaa hicho kinaelezwa kuwa kipo kwenye Huawei Mate 20 inayotazamiwa kutoka mwezi Oktoba katikati.

Vyanzo: The Verge, GSMArena

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|