WhatsApp ni moja kati ya mitandao ya kijamii maarufu sana. Mtandao huu hurahisisha mawasiliano baina ya watu haswa kwa kipengele chake cha kutuma na kupokea meseji
Ukiachana na kipengele hicho bado WhatsApp inajulikana kwa uwezo wake wa kuweza kupiga na kupokea simu. WhatsApp kama mtandao kwa sasa una watumiaji Bilioni moja duniani kote.
Mtu yeyote anaweza akajiuliza kuwa ni simu ngapi zinapigwa kwa siku kwa kutumia mtandao huo wa WhatsApp?
Kwa siku mtandao huo unasaidia simu milioni mia moja tena zile za sauti kuweza kupigwa. Hii ni namba kubwa sana, kumbuka simu hizi zinapigwa kwa siku tuu (pata picha kwa mwezi au hata mwaka mzima)
Hili ni jambo la kuvutia sana na inabidi iwe ni mfano wa kuigwa kwa makampuni mengine. Kumbuka huduma hii ya simu (za sauti) ilianzishwa katika mtandao huo wa WhatsApp mwaka jana (2015).
“Tumefurahi kwani watu wengi wameipokea vizuri huduma hii (kupiga simu kwa sauti) na tunajikita zaidi katika kuhakikisha tunaiboresha zaidi katika miezi inayokuja” – kampuni ilisema
Usije ukashangaa namba ya simu hizi inapanda kwa kuwa watumiaji wa App ya WhatsApp wanaongezeka kila siku. Pia huduma hii ni nzuri kwa kuwa inawasaidia watu kuongea na wapendwa wao (ndugu, jamaa na marafiki)
Hebu fikiria mtu anaweza akampigia mtu mwingine ambaye yuko nje ya nchi bila ya kulipia ngarama za ziada za nje ya nchi – safiii!
Ukiachana na hili la simu za sauti bado kampuni katika miezi kadhaa iliyopita iliripotiwa kuwa katika mchakato wa kuanzisha huduma ya simu za video – yaani utakua unamuona anaekupigia/unaempigia – katika App hiyo
WhatsApp ni moja ya App ambayo iko chini ya kampuni la Facebook. Facebook kwa sasa ndio mtandao wa kijamii wenye nguvu kwa sasa kuliko yote. Hivyo basi mengi yanaweza yakafanyika katika mtandao wa WhatsApp chini ya uangalizi wa Facebook