fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Mac Maujanja Picha Windows

Luminance HDR: Tengeneza Picha Katika Mifumo Ya HDR Na Programu Hii!

Luminance HDR: Tengeneza Picha Katika Mifumo Ya HDR Na Programu Hii!

Spread the love

Kama unapenda kupicha picha Luminance HDR ni kwa ajili yako. Hivi ulishawahi kupiga picha ambayo mwanga ukawa mdogo sana au ukawa mwingi sana?

Kwa mfano hata ukipiga picha mbele ya jua unaweza ukashangaa katika picha linatokea jua (kali) na mtu katika hali ya weusi ulipitiliza (kiasi cha kwamba unaweza usione sura ya mtu vizuri), na mara nyingine unaweza ukaona rangi ya nguo tuu.

SOMA PIA  Jinsi Ya Ku Share Mafaili Kati Ya iPhone, iPad na Mac Kupitia AirDrop!

Luminance HDR inaweza ikasaidia kwa kiasi kikubwa. Ukichukua picha hiyo hiyo uliyoipiga (ambayo jua linaonekana sana, na mtu anaonekana nguo) unaweza ukaibadilisha na kuwa picha ya kawaida ambayo mtu wa kawaida anaweza akaona kila kitu katika picha hiyo.

Mfano Wa Picha Iliyofanyiwa Manjonjo Na 'Luminance HDR'

Mfano Wa Picha Iliyofanyiwa Manjonjo Na ‘Luminance HDR’

Luminance HDR pia inaweza ikatengeneza mafaili mengi ya HDR kutoka katika picha moja. Licha ya hivyo pia inaruhusu kubadilisha rangi, kuizungusha, kuibadilisha saizi na ukishamaliza kuifanyia hayo yote unaweza ukaisevu

SOMA PIA  Jinsi Ya Kutuma Muziki Katika WhatsApp Ya iOs!

Programu hii pia inasapoti mafaili katika mfumo wa HDR na LDR.

Shusha WindowsBure

Shusha MacBure

Mpaka hapo kama una picha ambazo mwangaza wake haupo kawaida – yaani ni mwingi sana au mdogo sana – Programu (Luminance HDR) hii itakuwa ndio mkombozi wako.Kizuri ni kwamba inapatikana bure na pia kama programu nyingi za bure zilivyo wakati wa kuipakua itakuomba kuchangia (lakini unaweza kukataa na kuendelea kupakua).

SOMA PIA  Namna ya kuandika ujumbe haraka kwenye Gmail

Hongera kwa kujua maujanja haya, mwambie na mwenzio atembelee mtandao pendwa wa TeknoKona kila siku kwa habari kama hizi na zaidi ya hizi. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

TeknoKona Teknolojia Tanzania