WhatsApp kwa iOS imekuwa ikifanya mabadiliko mara kwa mara kwa kuongeza huduma mpya ama kufanyia mabadiliko fulani katika huduma za awali ili kuziboresha na kuwafanya watumiaji waendelee kupenda huduma hizi.
Watumiaji wa app hii katika iOS wamepata features mpya ambazo pamoja na mambo yote zitawasaidia watumiaji hawa kuweza kuamua picha muziki/sauti ama video kutoka kwa namba zipi za simu ama makundi yapi ya WhatsApp ziweze kuhifadhiwa katika simu zao.
iOS wanapata vipengele hivi baada ya WhatsApp ya kwenye Android kuanza kufanyiwa majaribio vipengele vipya kama vile namna maandishi yanavyoweza kutokea, ni wazi kwamba baada ya muda vipengele hivi vipya vitakuwa vinapatikana kwa Android pia.
Vipengele ambavyo vimeongezwa katika toleo jipya la WhatsApp ya iOS ni pamoja na uwezo wa kuchagua ni watu gani ambao wakikutumia mafaili ya picha muziki ama video yapakuliwe na kuhifadhiwa katika simu yako.
Huduma hii itasaidia watumiaji wa iOS kuweza kuwa na mamlaka ya juu ya nani na nani wawatumie picha muziki (ama sauti) au video kitu ambacho ni muhimu kama unataka kuzuia simu yako kujaa vitu ambavyo haupendi.
WhatsApp inazidi kubamba imekuwa ni moja ya app ambazo zinawatumiaji wengi sana, ikiwa imekwisha pitisha idadi ya watumiaji bilioni moja ni wazi kwamba simu janja bila WhatsApp sio simu janja bado.
Kwakuwa mabadiliko haya yanawaruhusu watumiaji pia kuamua picha katika makundi yapi ya WhatsApp ambazo zikiingia ziwe zinapakuliwa na kisha kuhifadhiwa katika memory ya simu.
Vipengele hivi vipya vinaleta mamlaka zaidi kwa watumiaji wa WhatsApp, hii ni wazi kwamba watengenezaji wa mtandao huu wanataka kuhakisha kwamba WhatsApp haichukiwi na watumiaji wake na badala wanataka kuona kwamba tunatumiwa app hii kwa furaha na manufaa.
Toleo hili la WhatsApp pia linakuja na kipengele kipya ambacho kinamruhusu mtumiaji kupata notification kuhusu WhatsApp kutoka app yenyewe na sio katika recent apps hii inamaana kwamba watumiaji wa mtandao huu katika jukwaa la iOS sasa wataweza kujibu ujumbe na simu za WhatsApp bila ya kuhitaji kwenda katika app husika.