Tulishaandika kuhusu matoleo yasiyo rasmi ya WhatsApp ambayo yanatengenezwa na watu ambao hawapendezwi na baadhi ya mipangilio (settings) ya app hiyo na pia wangependa kuona mambo mawili matatu ya kiutofauti zaidi. Matoleo haya huwa yanatolewa hasa hasa kwa watumiaji wa simu za Android.
Kusoma kwa undani kuhusu makala yetu yaliyopita bofya;
Baada ya WhatsApp kununuliwa na Facebook waliamua kufanya mabadiliko mbalimbali yakihusisha kuzuia apps za aina hizi ambazo si rasmi zishindwe kufanya kazi. Moja ya hatua waliyoweza kuifanya miezi michache iliyopita ni pamoja na kuwazuia watu wanaotumia apps zisizorasmi kupata huduma za WhatsApp kwa zaidi ya masaa 24.
Muda umeenda na watengenezaji wa toleo la WhatsApp Plus wameweza kutengeneza toleo linaloshinda zuio hilo la masaa 24, na pia katika toleo hili hata uwezo wa kupiga simu za WhatsApp unapatikana kama kawaida.
Sifa za Whatsapp Plus Reborn v1.80
- Badilisha muonekano wa WhatsApp (theme), rangi yake na ata ‘fonts’.
- Tuma mafaili kwa ukubwa wowote hadi kufikia MB 50
- Ficha habari zako za kupatikana ‘Online’ na ‘Last Seen’
- Tuma picha kwenye ubora mkubwa (Quality)
Kushusha APK ya WhatsApp Plus Anti-Ban (MB 24) bofya hapa -> (SHUSHA/DOWNLOAD) kama hapo pakisumbua unaweza pata faili hilo hapa pia (Drive)
No Comment! Be the first one.