Kwa wafanykazi au mtu yeyote ambae anapenda kuweka shughuli zake katika mpangilio fulani bila shaka atakuwa anafahamu kalenda ya Google ambayo kwa namna moja au nyingine anaitumia kuweza kuweka mpiango yake vizuri.
Katika siku 365 katika mwaka ni wazi kwamba sio siku zote utakuwa upo kazini au kwa akili ya kibinadamu utaweza kukumbuka ratiba zako zote kuwa unatakiwa uonane na mtu siku na saa fulani na hapo ndio teknolojia ya kutumia kalenda unayoiweza kuiona na kupanga mambo yako inapokuwa msaada.
Kuanzia sasa kwenye kalenda ya Google utaweza kuweka alama siku ambazo hutakuwepo (Out of Office) na hii ikimaanisha kwamba iwapo mtu atajaribu kukutafuta wewe katika siku hiyo au hizo siku umezinakili kwenye kalenda kuwa haupo basi atapata ujumbe kuwa hupatikani kwa siku hizo.
Mbali na kuwa na uwezo wa kuweka siku ambazo utakuwepo na hutakuwepo kazini lakini pia hapohapo kwenye kalenda ya Google utaweza kuweka muda unaopatikana (saa za kazi) na nje ya hapo mtu akijaribu kukutafuta atapata/ataona ujumbe “Hupatikani kwa muda huo” au ujumbe tofauti ambao utakuwa umeweka ili watu wakijaribu kukutafuta wauone mara moja.
Katika masasisho yajayo kwenye kalenda ya Google, wahusika wameweka wazi kuwa watatumia ujumbe wa sauti kumfahamisha kuwa mhusika hayupo/hapatikani. Teknolojia hii inafamika na wengi kama ‘Akili ya kufikirika’ (AI).
Vyanzo: Gadgets 360, TechCrunch