Katika teknolojia nyingi sana za miaka ya karibuni inatumia mfumo wa “Upeo usio halisi” katika vitu vingi tu vya kiteknolojia hasa kwenye simu janja na uhifadhi wa vitu hewani lakini yote hayo yakihitaji matumizi ya intaneti ili kufanikisha.
Wanasayansi wapo katika uundaji wa mfumo wa Artificial Intelligence (AI) au kwa tafsiri isiyo rasmi “Upeo usio halisi” ambao utakuwa ukitumika kama mfumo wa sasa unavyotumika lakini tofauti yake ikiwa ni haitakuwa inatumia intaneti katika utekelezaji wa majukumu yake.
Simu janja nyingi zilizotoka na zinazokuja karibu zote zimewekewa mfumo wa AI ambao unahitaji uwepo wa intaneti ili kuweza kufanya kazi katika namna tofauti tofauti ambapo inafanya kwa kiasi fulani bei ya simu janja ziwe juu iwapo imewekewa/inatumia mfumo wa upeo usio halisi.
Kwanini vifaa vingi vya kiteknolojia vina mfumo wa Artificial Intelligence?
Usalama wa kitu ndio furaha ya mtumiaji na kutokana na mambo ya udukuzi wa aina tofauti tofauti ilipelekea kwa mfumo wa upeo usio halisi uweze kuundwa ili kufanya kitu fulani kiwe na ulinzi wa aina yake. Kwa mfano dhahiri kabisa utaona Apple walivyoamua kutoa kitufe cha nyumbani na kuweka utambulisho wa uso (Face ID) kwenye iPhone X ambapo ili simu kufunguka lazima mfumo wa Artificial Intelligence utumike.
Jinsi Artificial Intelligence inavyofanya kazi.
Katika hali ya kawaida kama mtu anavyoambiwa jambo na kulitafakari kisha kulitolea maamuzi au ufafanuzi ndivyo hivyo hivyo upeo usio halisi unavyofanya kazi zake kwa kupitia katika madaraja mbalimbali kabla ya kutoa kile kinachotegemewa kifanyike au kitokee. Ufanyaji kazi wa upeo usio halisi unahitaji memori, nguvu ya kompyuta (ambayo ndani yake intaneti lazima itumike) na nishati (chaji, umeme, n.k).
Katika kile ambacho sasa hivi wanasayansi wanakishughulikia ni kuja na mfumo wa upeo uso halisi ambao utaweza kuwekwa kwenye simu janja, teknolojia ya kuhifadhi vitu hewani (cloud computing), roboti na kutoa usalama na usiri uleule ambao hivi sasa unapatikana kwenye artificial intelligence lakini bila kutumia intaneti.
Haijafahamika ni lini mfumo huo mpya wa ‘upeo usio halisi’ usiotumia intaneti utakamilika ila ni suala la muda tu na mfumo huo utakuwa tayari kutumika/kupatikana jambo ambalo litabadilisha kabisa mienendo ya wanateknolojia.
Chanzo: Gadgets Now
One Comment
Comments are closed.