Inawezekana ukawa umetuma maombi ya urafiki kwa watu wengi katika mtandao wa kijamii wa Facebook. Sasa utajuajuje nani amegoma kukubali au kukataa ombi hilo?
Kwa kufuatilia hiki mtandao wako pendwa wa TeknoKona unachokuletea, utakuwa na uwezo wa kuona nani na nani wamegoma kufanya chochote kuhusiana na ombi lako la urafiki ukiwa Facebook
Tuzifahamu Njia Za Kutumia
- Log in katika akaunti yako ya Facebook
- Chagua eneo la ‘Friends’ na kisha ‘See All’
Eneo La ‘See All’ Katika Marafiki - Chagua ‘View Sent Request’
Eneo La ‘View Sent Request’ Katika Marafiki - Mpaka hapo utakuwa na uwezo wa kuona ni nani amekuwa akipotezea ombi lako la urafiki. Kama unataka kufuta ombi hilo (kulisitisha), kwa urahisi kabisa inakubidi nenda juu ya ‘Friend Request Sent’ na kisha chagua ‘Cancel Request’
Mpaka hapo naona utakua ushajua nani amegoma au anapotezea kukubali ombi lako la urafiki sio? Tuandikie sehemu ya comment hapo chini kwamba hii umeipokea vipi?
TeknoKona Na Sisi Tupo Facebook Na Ukitu Like Hatuta kupotezea, Unaweza Uka ‘Like’ TeknoKona Hapa.
Usisahau kwamba TeknoKona tuna maujanja kibao ya kukupa kila siku, kwa hiyo usiache kutembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKona kila siku.Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Chanzo: Business Insider