Twitter sasa inataka kubadili muonekano wake wa tweets zake kuwa wa kipekee na kuweza kutofautisha kati ya mtu wa kwanza kuandika ujumbe (tweet) na wachangiaji wa ujumbe (replies).

Katika kufanikisha uharaka wa mambo mapya kujaribiwa na kundi la watumiaji wengi kabla ya kusambazo kwa wengine Twitter wameamua kuja na toleo spesheli la app ya mfano (prototype) rasmi ambayo itakuwa inapatikana kwa jina la Twttr.
Jina la Twitter litatumika kwa toleo rasmi kwa watu wote wakati Twttr itakuwa jina la toleo la app kwa ajili kufanya majaribio (Beta).
Kwa sasa toleo la Twttr linafanyiwa majaribio kwenye programu endeshi (operating system) ya iOS tu.
Muonekano mpya uliokwenye majaribio ni pamoja na kuweka lebo pale watumiaji wa Twitter wanapochangia ujumbe(tweet). Lebo izo ni kama following, author and mentioned ambazo kwa lebo ya following itaonyesha watu uliowafollow ambao wamechangia katika ujumbe(tweet), author itaonekana na muazilishi wa ujumbe husika na mentioned itaonekana kwa mtu aliejibiwa na mwandishi wa kwanza wa ujumbe(Author).
picha : techcruch
muonekano wa lebo zitakuwapo ndani ya tweet
Si kila mtu anaweza kupata mfano mpya wa majaribio lakini unaweza kuomba uwezeshwe na kujaza form zao za maombi kupitia HAPA