Fikiria unaweza ukawa unatumia simu yako ya iPhone kupiga picha na kurekodi video nyingi sana na huwa unazihifadhi katika hifadhi ya kimtandao ya iCloud.
Ni wazi kwamba picha na video nyingi zinakula nafasi sana hata ile ya kimtandao kwani iCloud inakupa GB 5 tuu ambazo ni bure, hapo nafasi ikijaa inabidi ununue nafasi nyingi zaidi ya kimtandao.
Kwa nini uingie gharama wakati unaweza kabisa kuhamisha baadhi ya vitu katika uhifadhi wa kimtandao mwingine? Kwa leo TeknoKona inakufundisha jinsi ya kuhamishia picha zako kutoka iCloud na kwenda katika Google Photos.
Kwanza kabisa ingia privacy.apple.com kwa kutumia kompyuta (usitumie simu) na kisha log in.

Kubali “Continue” ili kuendelea mbele

Baada ya kukamilisha hilo sasa unaweza kuchagua “Request to Transfer a Copy of Your Data” ili kuweza kuhamisha picha zako.

Yatatokea machagua ya juu ya namna jinsi taarifa hizo zinavyoweza kuhamisha na bila shaka hapo utakua ndio uwanja wako wa kufanya machaguo jinsi unavyotaka. Katika sehemu ya kuhamishia taarifa hizo chagua ‘Google Photos’

Ukishamaliza kufanya machaguo yote unaweza chagua neno ‘continue’ ili kuendelea mbele

Hapa inabidi uzingatie sana maana inawezekana pia Google Photos pia kukawa hakuna ujazo wa uhifadhi wa kutosha, hivyo basi kama hili likitokea jua wazi kwamba si taarifa zako zote ambazo zinaweza zikahama.

Ukurasa mpya utatokea na kukuambia kwamba uingie katika akaunti yako ya Google

Chagua “Allow” katika ukurasa ambao utatokea ili kuruhusu zoezi zima la kuhamisha taarifa hizo.


Baada ya hapo Apple itakuletea ujumbe wa taarifa kwamba huduma mpaka kukamilika itakuchukua siku 3 mpaka 7 na zoezi litakapo kamilika basi utapokea taarifa kwa kupitia barua pepe yako ya Apple. Maalizia kwa kuchagua “Confirm Transfers”

Namna hiyo mpaka hapo nadhani utakuwa tayari umeshaweza kufanikisha zoezi hili lote.
niandikie hapo chini katika sanduku la maoni je ni njia gani uliyokua unaitumia mwanzo kama ujazo uhifadhi wako ukijaa?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!
No Comment! Be the first one.