fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Apple apps iOS Maujanja Teknolojia

Zifahamu Keyboard 5 Za Mbadala Kwa Ajili Ya iPhone!

Zifahamu Keyboard 5 Za Mbadala Kwa Ajili Ya iPhone!

Spread the love

Wakati iOS na Android zimekua kwa kiasi kikubwa na zina vipengele mbalimbali vinavyo fanana lakini kile kikubwa cha kuwatofautisha ni keyboard.

Simu za android ziliwezesha keyboard kutoka kwa watu wengine ambao waliweka application (keyboard)  hizo katika google playstore, Apple hawakufanya hivyo toka mwanzo. Tangia iOS 8 itoke  Apple walifungua mlango kwa watengenezaji wa keyboard  hii imechangia mpaka baadhi ya watengenezaji wa keyboard katika Android kutengeneza zile za iPhone na iPad.

safari-iphone-tips-big-keyboard

KeyBoard Ya Kawaida Na Iliyo Zoeleka Katika iPhone Na iPad

Kazi kubwa imefanyika na Teknokona kutofautisha mchele kutoka kwenye maharage. Zifuatazo ni keyboard nzuri zaidi katika iOS.

Fleksy

fleksy-keyboard

Hii Inauzwa Dola 0.99 Za Kimarekani Katika AppStore

Keyboard ya Fleksy ni nzuri sana na inatoa huduma katika vipengele vingi kama vile kuotea, kumalizia maneno, na kurekebisha maneno (gestures, auto-correction, text prediction, and size options). Inaweza pia kukusoma jinsi unavyandika katika barua pepe (E-mail) zako na mitandao ya kijamii.

Kama maelezo hayo hayatoshi  Fleksy bado inatoa huduma ya vitu kama emoji, GIFs na uwezekano wa kuandika kwa kutumia mkono mmoja. Kitu kimoja tuu ambacho haifanyi ni kuandika juu ya kioo ili maandishi yatokee. Lakini kwa dola moja tuu ya kimarekani sidhani kama unaweza lalamika.

Minuum

minuum_final_ios8

Hii Inauzwa Dola 3.99 Za Kimarekani Katika AppStore

Minuum ina bei kubwa kuliko Fleksy. lakini inafanya vitu ambavyo keyboard nyingine haziwezi fanya. Kikubwa ni kwamba ina uwezo wa kuficha keyboard yote kwa chini kabisa na kutengeneza mstari mmoja chini ya skrini. Kwa kutumia vipengele vyake vya kuotea na kumalizia maneno bado inaweza kukusaidia kuandika maneno kwa kugusa skrini yako tuu.

Wengine wanaweza pata shida kujua kuitumia mara moja tuu, lakini kila kitu ni kujifunza tuu ili kuelewa. Pia hii keyboard ya minuum inakusaidia kuweza kuongeza kamusi yako kwa kutumia maneno yako mwenyewe. Na kama unapenda sana emoji Keyboard hii itafanya yote hayo kwa ajili yako.

SOMA PIA  Kwa Ufupi: Habari Mseto za Wiki!

SwiftKey

swiftkey-banner

Hii Inapatikana Bure Katika AppStore

SwiftKey ni keyboard nzuri na mbadala kwa jaili ya iOS pia ni ya bure. Tangia mwanzo ilikua inapendwa sana na watumiaji wa Android.

Sio tuu inaweza otea maneno yako na kumalizia baadhi ya meneno kwa ajili yako pia itasoma namna au jinsi unavyo tuma meseji kwa katika mitandao ya kijamii (Facebook, Twitter, Gmail, Evernote, na akaunti za namba za simu ) ili kukusaidia katika kuandika.

Pia keyboard  hii ni moja kati ya zile nyingi ambazo zinaweza kukuwezesha kuandika kwa kutumia mkono mmoja.

Swype

EN-4.0-Swype

Hii Inauza Dola Za Kimarekani: $0.99 Katika AppStore

Kama jina linavyoonyesha Swype ilikua ni moja kati ya zile keyboard za mwanzo katika Android ambayo inamuwezesha mtu kuandika juu ya skrini ili maneno yatokee. Tangia Apple waruhusu watu kutengeza keyboard kupitia mlango wa nje, Swype ikabisha hodi katika iOS.

SOMA PIA  Bustani ya kidigitali yenye sauti mbalimbali za matunda yaundwa #Teknolojia

Wakati keyboard zingine zinafanya juu chini ili ziweze otea maneno yako au kumalizia maneno yako, Swype inafanya kila namna ili mtumiaji wake aweze kuandika neno analo lihitaji pale anapolihitaji na hichi ndio kitu ambacho kinafanya vizuri, tena vizuri sana.

Pia ina kamusi kwa ajili ya kuongeza maneno na pia inakupa nafasi ya kuchagua mionekano (‘theme’) mabali mbali

ThemeBoard

THEMEBOARD

Hii Inapatikana Bure Katika AppStore

Kubwa kuhusu hii keyboard ni kwamba imejikita zaidi katika ‘theme’ ndio maana ikaitwa ‘ThemeBoard’. Keyboard hii ni bure na pia inatoa mionekano mbali mbali ya bure lakini vitu vingine bomba vitaku gharimu kitu kidogo

Themeboard haina mambo ya ajabu sana kwani itatoa huduma sawa na SwiftKey au Fleksy.

Jinsi Ya Ku ‘Install’ Keyboard Katika iOS

  1. Shusha Keyboard unayoitaka katika AppStore
  2. Katika iPhone au iPad Ingia katika menu ya setting kisha nenda General -> Keyboard -> Add New Keyboard
  3. Chagua ile Uliyo ishusha
  4. Keyboard ikitokea katika App mfano WhatsApp bonyeze kialama cha dunia kile kisha chagua ile unayoitaka

Wazo lako ni muhimu, ningependa kusikia kutoka kwako pia tafadhali ungana nasi kupitia kurasa zetu za Facebook ,Twitter, Na Instagram

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania