Kuna kipindi tulikuandikia kuhusiana Google, Microsoft na Apple katika mpango wao wa kuhakikisha kuwa watu wanakua hawaandiki nenosiri mara kwa mara wakiwa wanatumia kifaa kimojana kuhamia katika passkeys.
Unaweza kusoma zaidi kuhusuiana na makala hiyo juu ya passkeys >>HAPA<< lakini kwa sasa ni zamu ya Google katika huduma zake za Android na Chrome katika kuhakikisha kuwa inawezesha jambo hili.
Ni wazi katika vifaa vya Apple hili limeshafayika kwa kiasi chake maana wale wanatumia teknolojia ya password auto-fill, kwa Google kitakachofanyika ni kwamba watakua na huduma hii ya Passkeys ili kuhakikisha kuwa kuna usalama wa juu wakatik mtu akiwa anapitia katika huduma na mitandao yake.
Kingine ni kwamba kinacho onekana ni kwamba Passkeys ndio njia salama zaidi kuliko kuandika neno siri upya wakati ukiwa unaingia kila katika huduma husika.
Kingine ni kwamba Passkeys hizo haziwezi kujirudia katika kuingia katika sehemu moja mara mbili, ni kwamba ukiitumia mara moja tuu inabadilika.
Passkeys sio huduma ngeni na inatumika kwa mifumo endeshi mingi tuu, na vile vile inaweza kutumiaka katika tovuti (website) na App mbalimbali.
Hapa kizuri ni kwamba passkeys hizo zitakua zinatumika ndani ya tovuti mbali mbali na App na zitakua zimehifadhiwa katika kifaa (simu janja)
Uhifadhi huo utafanyika vyema maana hifadhio ni Google Password Manager na utaweza kutumika vyema katika vifaa vya Android na vile vinavyotumia Chrome.
Ningependa kusika kutoka kwako, naindikie hapo chini katika eneo la comment,je hili umelipokeje? Je hujachoka kuandika neno siri mara kwa mara katika kifaa kimoja?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.