Store hiyo mpya ya Microsoft iitakua ni mahususi kwa magemu ya kwenye simu na hii itakua ni mshindani mkubwa kwa Apple na Google kwa sasa.
Magemu hayo yatakua ni yale ambayo yana chapa ya Xbox (au yanapatikana kwa kiasi kikubwa katika Xbox) kutoka katika kampuni ya Microsoft. Fikiria magemu yale ukiwa unayapata katika simu janja yako ikiwa ni Android au iOS.
Ni wazi kwa sasa soko la magemu duniani limetekwa katika simu janja, maana ndipo ambapo panaingiza hela nyingi kwa mwaka ukilinganisha na vyanzo vingine vya magemu.
Hili limetokea mara tuu baada ya kampuni ya Microsoft kuinunua kampuni ya Activision Blizzard ambayo ina magemu mengi sana katika simu za Android na iOS.
Kwa upande wa Microsoft wenyewe wanasema wanataka wausogeze ule uzoefu wa kucheza magemu kwenye Xbox katika simu janja— na hili likiwa ni wazo zuri.
Kingine ni kwamba kuna watumiji wengi sana wa simu janja (pengine kuliko vifaa vingine) hivyo hata namba ya watumiaji wa magemu (na huduma za magemu hayo) itaongezeka kwa kiasi kikubwa.
Kitakachofanyika hapa ni kwamba magemu ya Xbox kwa njia ya simu janja yatakua hayapatikani tena katika masoko ambayo tumeyazoea yaani Google Play Store na App Store.
Stoo mpya kabisa itaingia katika soko na ikiwa ni spesheli kabisa kwa ajili ya magemu ya Xbox pekee, pengine inaweza ikaitwa Microsoft’s Mobile Gaming Store.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika uwanja wa comment, je utaweza kuachana na sehemu zingine na kuanza kuchukua magemu katika stoo hii na kuanza kucheza?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.