Sasa unaweza ukawa nin mtumiaji mzuri wa mtandao wa WhatsApp lakini vipi kuhusu kipengele kipya cha Community? Je umeshaanza kukitumia? Na kama bado je kipengele hicho ni mahususi kwa ajili gani?
Kama unavyoona makundi katika mtandao wa WhatsApp inabidi kuwa na namba ya mtu ili kumuingiza katika kundi lakini kupitia community kutakua na maelefu ya watu kuingia katika community moja
Kingine ni kwamba ndani ya community moja ambayo ina maelfu ya watu kutakua na makundi mbalimbali (yenye mada tofauti tofauti).
Yaaani kwa mfano hapa tunaweza tukawa tuna community tunayoiita TeknoKona na ndani yake hata tukawa na makundi mengine mengi mfano (TeknoKona Tanzania, TeknoKona Kenya n.k)
Wakati ukiwa katika kipengele hicho namba yako ya simu haiwezi kuonekana (itafichwa) kwa watu, labda kwa wakuu (admin) wa makundi na watu ambao uko nao katika kundi moja.
Ukifuatilia sana utagundua kuwa hakuna utofauti mkubwa sana na makundi ya kawaida ila ni kwamba kwa community imepewa uwezo mkubwa hata wa kumeza makundi mengi ndani yake.
Mpaka katika kipengele hiki kipya kutakua na ulinzi na usalama ule wa end-to-end encryption kama tulivyozoea kwa huduma zingine za WhatsApp.
Community ni njia rahisi ya kuweka makundi mengi yaw echini ya mwamvuli mmoja. Kama kawaida ya mtandao huu wa WhatsApp, mara nyingi huwa wanafanya maboresho na kuleta vipengele vingi ili kujihakikishia kuwa wanabaki kuwa namba moja katika kutoa huduma hiyo
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je umeshaanza kutumia huduma hii? Kama bado je uko tayari?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.