Mtandao mkubwa wa kijamii upo njiani kuleta teknolojia ya intaneti yenye kasi mara 4o zaidi ya teknolojia ya 4G.
Teknolojia hii inafanyiwa utafiti ili iweze kutumika kupeleka intaneti katika sehemu zisizofikika kirahisi huu ni mpango wa Facebook unaolenga kuwapa huduma ya intaneti watu wa vijijini.
Facebook imeuthibitishia mtandao wa VERGE kwamba unafanyia kazi teknolojia mpya ya intaneti ya kasi na kusema kwamba mpango huu ni mmoja wa mipango ambayo ipo chini ya maabala yake iliyopewa jina la Connectivity Lab.
Connectivity Lab ni maabara ambayo inafanya tafiti mbali mbali za jinsi ya kuwapatia watu intanet katika maeneo yasiyo rahisi kufikika, zipo teknolojia nyingine ambazo zinafanyiwa utafiti na kituo hiki mojawapo ni ile ya intanet kurushwa na ndege zisizo na rubani maarufu kama drones.
Facebook imekuwa mstari wa mbele saana katika kutaka kuwapatia huduma ya intanet watu ambao hawana huduma hii hasa watu wanaoishi katika maeneo ya vijijini, na imekwisha fanya mambo mengi kutimiza azma yake hii ikiwa na pamoja kuleta huduma ya freebasics.
Ni wazi kwama freebasics imeshindwa vita baada ya kupigwa vita sana na tayari imeanza kufungiwa kwa baadhi ya nchi kama India ambako ndiko kulikua kama sehemu ya mfano, Uzuri ni kwamba inaonekana Facebook walikua na mpango mbadala na bila shaka hii teknolojia ni moja ya mipango mbadala ya freebasics.
Teknolojia hii inategemewa kuweza kusafirisha data katika mawimbi yenye wavelength ndogo kiasi cha milimita moja, mawimbi haya ambayo yatakuwa na freequency kubwa saana na haijawai wezekana kusafirisha data katika mawimbi kama haya(ingawa ipo kampuni moja ambayo imeyafanyia majaribio mawimbi kama haya).
Changamoto zipo nyingi katika ugunduzi huu kwa mfano mawimbi ambayo yana wavelength ndogo kama hii hayatakuwa na uwezo wa kupenyeza vizuizi kama ukuta au hata maji katika hewa hivyo itahitaji teknolojia ya ziada kufanyikisha hilo. Changamoto nyingine ni kwamba mawimbi yenye wavelength fupi yatahitaji kupata nguvu nyingi katika antena zinazorushwa hii kibiashara sio nzuri kwa kuwa itazidisha gharama za uzalishaji.
Yote kwa yote tunategemea mwanzo huu utakuwa mwanzo wa ugunduzi ambao utasaidia watu wengi zaidi kupata huduma za intaneti bila ya vikwazo vyovyote.
No Comment! Be the first one.