fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Apple IPhone

Uko Tayari Kwa iPhone 5se Ya Pinki?

Uko Tayari Kwa iPhone 5se Ya Pinki?

Spread the love

Kampuni la Apple halijalala kabisa, bado linaendelea kutoa bidhaa tofauti tofauti kuhakikisha kuwa wateja wake wanaridhika kutokana na bidhaa zao. Apple mbioni kutoa iPhone yenye ukubwa wa inchi 4 (iPhone 5se) katika rangi ya Pinki

Ndio rangi ya pinki, hii itakuwa ni ya kitofauti kwani kampuni halikuwahi kutoa simu yenye rangi hii katika jamii. Japokuwa ni kitu kipya lakini nina imani kitapata muamko mkubwa kwani kuna watu wanpenda rangi rangi. Lakini pia kumbuka rangi nyeusi, nyeupe na gold zimeshazoeleka sana katika simu

iPhone 5se ambayo Apple imependelea iwe katika rangi ya pink inayoenda kwenye nyeupe, pia itakuja katika rangi ya silva na  ya kijivu. Simu hizi zitakuwa na umbo dogo ukilinganisha na hizi za matoleo ya iPhone 6.

iphone-5se

Huku ripoti zikisema kuwa simu hizi zinazokuja zitakuwa na prosesa ya A8 au A9, kamera ya MP 8 ambayo itakuwa inasapoti picha za ‘live’. Pia simu hizi zitakuwa na toleo la Siri ambalo lina maboresho. Hii ni kwa kutaja mambo machache tuu

Pia kuna hatihati kubwa kuwa simu hizi zitakuwa na prosesa ya A9 licha ya A8. Baadhi ya ripoti zinasema kuwa iPhone 5se haitakuwa na toleo jingine kwani prosesa ya A10 itakuwa spesho kwa toleo la iPhone ambalo linasubiriwa kwa hamu (iPhone 7)

SOMA PIA  Kimemeshi kipya cha kuchaji AirPods

Pia taarifa katika mtandao wa Mixpanel inasema kuwa; asilimia 32.23 ya watumiaji wa iPhone wanamiliki iPhone 5, iPhone 5C au iPhone 5s, ambazo zote zina kioo cha inchi 4. Tangia iPhone za zamani (matoleo ya zamani) zimeachwa nyuma katika ‘specification’ na mambo mengine mengi hivyo zinaenda nje ya soko. Mtu anaweza akasema simu mpya ya iPhone 5se inaweza ikawa ndio jibu kwani itakua ndogo kama zile zingine na kuwa na mambo yote ambayo yanapatikana katika simu kubwa (iPhone 6)  za iPhone

SOMA PIA  Apple yaongoza mauzo ya saa janja robo tatu ya 2017

Apple wanaamini kuwa watatangaza simu hii ya iPhone 5Se katika event spesheli  mwezi machi mwaka huu  na kuiingiza sokoni simu hiyo mwanzoni mwa mwezi machi mwaka huu

Tuambie unaichukuliaje rangi hii. Je unahisi wateja wengi watakuwa ni wa jinsia ya kike? Tuandikie sehemu ya comment hapo chini. Kumbuka kutembelea mtandao wako pendwa kila siku. Mwambie na mwenzako kuhusu iPhone hii.TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania