fbpx
apps, Teknolojia, Usalama

WhatsApp: Msg ulizozifuta kuweza kusomwa tena #Utafiti

whatsapp-msg-ulizozifuta-kuweza-kusomwa-tena-utafiti
Sambaza

Tafiti zinaonyesha kuwa kuna uwezekano wa zile msg ulizozifuta kwenye WhatsApp kuweza kusomwa tena.

Kutokana na utafiti ulifanywa na  Jonathan Zdziarsk umeonyesha kuwa pale unafuta msg za kwenye WhatsApp ukitegemea kutoziona tena, sio hivyo kama ulivyotegemea kwani msg hizo ni kwamba huondoka kwenye mbele ya macho yako lakini msg hizo zinabaki kwenye memori ya simu na zimawezekana kupatikana na kusomwa tena kwa kutumia app fulani.

INAYOHUSIANA  Maana ya "i" kwenye bidhaa za Apple #Teknolojia
Kufanya 'backup' ni muhimu lakini haimanishi mambo yako kwenye WhatsApp yapo salama.
Kufanya ‘backup’ ni muhimu lakini haimanishi mambo yako kwenye WhatsApp yapo salama.

Kwa wale wanatumia vifaa kutoka Apple wanatumia Forensic trace inafuatilia msg zote zilizofutwa au zilizokusanywa pamoja na kuwekwa mahali fulani. Msg hizo kwa kutumia Forensic trace zinaweza kurudishwa na kuweza kuonekana kama awali hata kama ulizifuta miaka mingi iliyopita.

Hakuna app itakayoweza kufuta kabisa msg zako ila cha msingi ni kujua kwamba pale unapoamua kufuta msg zako kwenye WhatsApp hazifutiki kabisa ila kuna mahali zinakuwepo na mtu ambaye atakuwa na access ya kutumia simu yako basi anaweza akarudisha msg hizo na kuweza kusomeka kama hapo awali.

Msg zote za kwenye WhatsApp zinahifadhiwa kwenye Database hata kama ukizifuta mtu anaweza akazipata na kuzisoma.
Msg zote za kwenye WhatsApp zinahifadhiwa kwenye Database hata kama ukizifuta mtu anaweza akazipata na kuzisoma.

Kitu cha kuzingatia

  1. Yeyote yule mwenye uwezo wa kupata acess kwenye simu yako iwapo kama ataijua password yako, pattern kwenye simu yako ataweza kutengeneza ‘backup’ na kuweza kuviona kwa hapo baadae. Ni muhimu kuficha password yako na kuwa nayo wewe tu.
  2. Iwapo mtu ataweza kuingia kwenye kompyuta yako anaweza akacopy kutoka kwenye simu yako, kufungua mafaili yaliyofungwa na kisha kuyatuma kwenye barua pepe yake na kuweza kufuatilia mazungumzo yako na yeyote yule uliyewasiliana nae kuptia WhatsApp.
INAYOHUSIANA  Jinsi ya Kupakia WhatsApp yenye Ladha Tofauti kwenye Simu yako

TeknoKona inashauri kuwa makini na ukuaji wa utandawazi ili kuweza kujiweka mahali salama.

Vyanzo: Telegraph, Unilad, Zdziarski’s Blog of Things

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|