fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Apple Teknolojia

Apple na wafanyakazi ambao hawajachanja chanjo ya UVIKO-19

Apple na wafanyakazi ambao hawajachanja chanjo ya UVIKO-19

Spread the love

Dunia nzima bado inapambana na janga la virusi vya Corona ambalo mpaka sasa limeshagharimu mamilioni ya maisha ya watu ulimwenguni kote.

Makampuni mbalimbali duniani yameboresha sera zao kama moja ya kukabiliana na janga la UVIKO-19 ambapo Apple imebadilisha mbinu za kufahamu hali za kiafya za wafanyakazi wao katika suala zima la virusi vya Corona.

SOMA PIA  Je simu za mkononi zinasababisha kansa ya ubongo? Utafiti mpya waja na majibu

Ingawa haijalazimisha lakini Apple imekuwa ikiwasukuma wafanyakazi wake waweze kupata chanjo ya virusi vya Corona ambapo kwa wale ambao hawajachanja na wanatoka na kwenda kuzunguka kwenye maduka ya rejareja basi wao watapimwa mara kwa mara kufahamu iwapo wapo salama dhidi ya UVIKO-19 ama la!.

UVIKO-19

Wafanyakazi wa Apple ambao wameshachoma chanjo ya UVIKO-19 watakuwa hawaangaliwi mara kwa mara kulinganisha na wenzao ambao hawachanjwa.

Facebook, Google pamoja na makampuni mengi makubwa kwenye ulimwengu wa teknolojia haijawabana wafanyakazi wake kuhusu suala zima la chanjo ya virusi vya Corona halikadhalika kwa Apple ingawa wao wameanza kuomba taarifa iwapo wamechanjwa au la tangu Septemba hii ianzie.

SOMA PIA  Septemba 14: Apple wathibitisha shughuli ya uzinduzi wa bidhaa zao

Kutoka idara ya wafanyakazi, usalama kazini nchini Marekani hivi karibuni makampuni makubwa yatalazimika kufanya iwe ni lazima kupata taarifa za wafanyakazi wao iwapo wameshachanjwa chanjo ya UVIKO-19 au la! Au iwe inawapima kila wiki. Vipi ewe msomaji wetu mambo yakoje nchini mwako?

Kumbuka kufuatilia TeknoKona ili uweze kuhabarika halikadhalika kuelimika kuhusu teknolojia.

Vyanzo: Engadget, mitandao mbalimbali

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania