fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

apps iOS Teknolojia whatsapp

Kipya kuhusu uwezo wa jumbe za WhatsApp kutoweka kwenye iOS

Kipya kuhusu uwezo wa jumbe za WhatsApp kutoweka kwenye iOS

Wengi wetu tunaotumia WhatsApp tunaweza kuwa tunafahamu kipengele kinachowezesha ujumbe alioutuma kwenda kwa mtu/ndani ya kikundi kufutika baada ya muda fulani kupita hii ikihusisha Android na iOS.

Mtu anaweza kukutumia ujumbe kwenye WhatsApp lakini baada ya muda fulani kupita ukashaangaa kutouona tena basi usije kushangaa ila tuu wewe fahamu kuwa ameruhusu jumbe zake kuja kwako au kenye kikundi zitoweke baada ya wiki moja. Kufahamu zaidi kuhusu kutoweka kwa jumbe kwenye WhatsApp BOFYA HAPA.

Kipengele cha jumbe kuweza kutoptea kililetwa machoni pa watu mwezi Novemba 2020 na tangu hapo kimekuwa kikifanyiwa maboresho.

Sasa kwenye iOS kuna maboresho mawili yanayohusisha WhatsApp. Mosi, umeongezeka upana wa kile ambacho kinakuwa kimetumwa  (picha au picha jongefu) aliyetumiwa kuweza kuona kabla ya kufungua kitu husika kwa ajili ya kuona kwa ukubwa zaidi.

Pili, awali kwenye iOS kipengele cha uwezo wa jumbe kuweza kutoweka ndani ya makundi kwenye WhatsApp ulikuwa umewezeshwa kwa kiongozi/viongozi wa kundi pekee lakini hilo sasa linabadilika kwani kwa mujibu wa toleo la 2.21.71 inaonyesha kuwa mtu yeyote yule ndani ya kikundi husika anaweza kuruhusu kipengele hicho kwa jumbe zake kutoweka kuanzia muda huo ambao atakuwa amekiwasha mpaka hapo atakapokizima.

kutoweka

WhatsApp toleo 2.21.71 likonyesha yalioboreshwa kwenye programu tumishi husika upande wa iOS.

Je, kinapatikana wapi?

Ukitaka kufanya kuruhusu jumbe unazotuma ndani ya kikundi zidumu kwa siku saba tu hata kama wewe si kiongozi wa kikundi basi huna budi kutembelea mpangilio uhariri wa taarifa za kundi na huko ndipo utaweza kuwasha ama kuzima kitu hicho.

kutoweka

Mtu yeyote yule ndani ya kundi kupitia WhatsApp kwenye iOS anaweza kuruhusu kipengele cha jumbe zake kutoweka.

WhatsApp wapo mbioni kuruhusu maboresho hayo upande wa Android na usipitwe kufahamu mengi na ya kina kuhusu kipengele hiki kwenye makala yetu ijayo.

Vyanzo: Gadgets 360 pamoja na mitandao mbalimbali

SOMA PIA  iOS 14 imewafikia watumiaji kwa asilimia ngapi mpaka sasa?
Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania