fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

apps Teknolojia Twitter

Maboresho mbalimbali kwenye Twitter

Maboresho mbalimbali kwenye Twitter

Spread the love

Moja ya mtandao wa kijamii ambayo haina watumiaji wengi duniani ni Twitter lakini imekuwa kwenye ushindani bila kusahau maboresho ambayo yanalengakuufanya kupata wateja wapya lakini kulinda kutopoteza ambao tayari wana akaunti.

Inawezekana ukawa una akaunti Twitter lakini si mtumiaji wa mara kwa mara na kuna wengine ndio mtandao wa kijamii ambao anaperuzi mara nyingi zaidi ndani ya siku moja. Kiukweli, Twitter imekuwa ikifanyiwa maboresho ambayo mbali na kulenga usalama wa akaunti za wateja wao lakini pia wameweka nguvu kwenye kuvutia zaidi.

SOMA PIA  Bongoline: Je Watanzania tumevutiwa?

Yapo maboresho akdha wa kadha yanayofanyika kwenye Twitter na kufanya kuvutia hata kwa wale ambao si wapenzi wa kupeuzi kwenye mtandao huo wa kijamii mara kwa mara. Maboresho hayo ni:

Uwezo wa kuficha machapisho. Twitter wanafikiria kuwezesha watumiaji wa mtandao huo wa kijamii uwezo wa kuficha machapisho ambayo yana siku 30, 60, 90 au hata mwaka mwaka mzima tangu yaende hewani. Machapisho hayo yatakuwa yanaonekana kwa aliyapeleka hewani tu na si kwa mtu mwingine iwapo ataruhusu mpangilio huo.

kwenye Twitter

Uwezo wa kuficha machapisho ya zamani kwenye Twitter.

Kuficha machapisho uliyotokea kuyapenda. Watumiaji wa Twitter watakuwa na uwezo wa kuweza kupanga nani, watu au kikundi kuweza kuona machapisho ambayo yule unayemfuata. Mfano sisi TeknoKona tunaweza kupenda machapisho mbalimbali ya Tecno Tanzania, Tume ya TEHAMA Tanzania sasa inawezekana kuchagua iwapo wewe unayetufuatilia kujua kuwa tumependa chapisho la mtu/kampuni fulani.

SOMA PIA  WhatsApp Kuruhusu Kujiunga Katika 'Video Call' Za Makundi!

Kuondoa watu wanaokufuata. Unaweza ukawa una watu ambao “Wanakufuata” kwenye Twitter na pengine ungependa kuwapunguza/kuwaondoa; hiki ni moja ya kipengele ambacho Twitter kukileta ambapo pia imeweka kwenye majaribio uwezo wa mtumiaji kuweza kumzuia mtu/watu kuona machapisho yake.

kwenye Twitter

Majaribio ya kipengele cha kuondoa wanaokufuata kwenye mtandao wa kijamii wenye watumiaji wachache bila ya “Kuwazuia”.

Uwezo wa kujiondoa lwenye mazungumzo. Tunafahamu vyema kuwa inawezekana kutajwa kwenye Twitter mathalani umeandika kitu halafu mwishoni ukamalizia na @teknokona. Kimsingi yule anayekutaja ndio mwenye uwezo wa kumuondoa aliyemtaja kwenye chapisho lake lakini hilo mbioni kubadilika; ukinitaja nitakuwa na uwezo wa kujiondoa kama nikitaka.

SOMA PIA  Jinsi Ya Kulazimisha Kushusha Gemu Ya 'Pokemon Go' Kwa Android Na iOS!

Haya sasa unayazungumziaje hayo yaliyoelezwa hapo juu? TUngependa kusikia maoni yako kutoka kwako msomaji wetu. Kumbuka kufuatilia TeknoKona ili uweze kuhabarika halikadhalika kuelimika kuhusu teknolojia.

Vyanzo: Gadgets 360, Engadget

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania