Ving’amuzi vya DSTV ni moja ya visimbuzi ambavyo watu wengi kwenye nchi za Afrika wanavitumia kuweza kupata chaneli mbalimbali duniani kwa lengo la kuhabarika, kuelimika, kuburudika, n.k ambapo teknolojia imeendelea kubadilika mpaka kufikia kuwa na sehemu ya kuchomeka USB ama flash.
Nina imani kama utakuwa ni mtu unayependa kukijua kifaa cha kielekroniki kabla ya kukiunganisha kwenye umeme basi utakuwa umeona kuwa bidhaa hiyo ina sehemu ambayo inaruhusu kuchomeka memori ya nje au kwa Kiingereza “Flash Disk Drive” au waya unawezesha kuchaji simu, tabiti.
Sasa kuna kitu kimoja kwenye king’amuzi cha DSTV kikawa kimekuacha na maswali kidogo; suala la kwamba ukichomeka memori ya zida kwa ajili ya kuweza kuangalia sinema, picha jongefu za muziki na mengineyo inakuwa haisomi lakini ukichomeka waya wa kuchaji simu (USB) kwenye rununu umeme unaingia. Je, ni kwanini ving’amuzi vya DSTV havikubali flash disk?
Jibu ni DSTV hawajaruhusu memori ya ziada (FDD) kuweza kutambulika kwenye king’amuzi LAKINI inawezekana kutumia sehemu hiyo kwa ajili ya kuchaji simu pamoja na vifaa vinginevyo vya kiganjani.
HIyo ndio JE, WAJUA?! Sasa tufahamu tuu tunaweza kuchaji rununu, tabiti kwenye king’amuzi cha DSTV na si vinginevyo. Sisi ndio TeknoKona, tufuatilie kila leo kwa habari mbalimbali zinazohusu teknolojia.
Chanzo: DSTV