fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Teknolojia

Fahamu Skendo Kubwa ya Kampuni ya Magari ya Volkswagen Inayohusisha Kudanganya Kwa Kutumia Teknolojia

Fahamu Skendo Kubwa ya Kampuni ya Magari ya Volkswagen Inayohusisha Kudanganya Kwa Kutumia Teknolojia

Spread the love

Kampuni ya magari ya Volkswagen imejikuta kwenye skendo kubwa sana ambayo hadi kufikia muda huu imesababisha kushuka kwa thamani za hisa zake kwa zaidi ya asilimia 60%. Kampuni hiyo imeshutumiwa na shirika la viwango la Marekani ya kwamba limekuwa likitumia teknolojia kudanganya viwango vya utoaji wa gesi haribifu kwa mazingira kwenye magari yake.

Wadanganya mashirika ya viwango vya ubora wa injini kwa kufanya ionekane baadhi ya magari yake ni bora na mazuri kwa mazingira kuliko hali halisi. Na uongo wote umefanyika kwa kutumia teknolojia tuu.

Gari ya Volkswagen ikiwa imeunganishwa katika mitambo ya uchunguzi wa viwango vya utoaji gesi

Gari ya Volkswagen ikiwa imeunganishwa katika mitambo ya uchunguzi wa viwango vya utoaji gesi

Elewa udanganyifu huu kwa maneno machache;

SOMA PIA  Go Green; App mahususi kwa ajili kukupa dondoo jinsi ya kutunza vitu mbalimbali

Kila injini ya gari huwa inatoa hewa chafu kama sehemu ya utendaji kazi wa injini. Kuna viwango vya ubora wa injini vilivyowekwa na mataifa mbalimbali kwenye nchi zao kuruhusu kiasi cha hewa/gesi chafu inayotolewa na injini za magari.

Kampuni ya Volkswagen imefanya nini hasa?

Kampuni hiyo kutumia chipu za kompyuta zilizopo kwenye baadhi ya magari hayo walifanikiwa kuyawezesha magari hayo kutambua pale ambapo yanaunganishwa na mitambo ya kugundua kiwango cha utoaji wa gesi ya Nitrogen oxide. Yakishatambua ya kwamba yameunganishwa na mitambo hiyo basi yanafanya injini ijiendeshe katika hali ambayo inatoa kiwango kidogo zaidi cha gesi hiyo ukilinganisha na pale ambapo yanakuwa yanatumika barabarani.

Magari ya injini zinazotumia mafuta ya diseli ndiyo yaliyo na teknolojia hiyo ya udanganyifu. Inasemakana magari zaidi ya milioni 11 ndiyo yenye udanganyifu huo na itaitajika zaidi ya shilingi Trilioni 14 kwa ajili ya kuyarudisha magari yaliyonunuliwa kabla na kuyafanyia maboresho.

Hali mbaya ni mbaya kiasi gani?

SOMA PIA  Na hii ndio simu janja Samsung Galaxy A03 Core

Kwa nchini Marekani tuu inasemakana ya kwamba kuna magari zaidi ya 480,000 yaliyouzwa kati ya mwaka 2008 na 2015 yaliuzika kupitia vyeti vya usalama wa mazingira vilivyopatikana kwa udanganyifu huo. Yaani ingefahamika mapema basi ‘model’ au aina ya magari ambayo yalipata vibali kuuzika nchini Marekani yasingefanikiwa kufaulu kupata vibali na kama yangepata basi yalitakiwa kupigwa ushuru mkubwa sana.

Martin Winterkorn, Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo ambaye anategemewa kujiudhuru nafasi yake muda wowote kuanzia sasa

Martin Winterkorn, Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo ambaye anategemewa kujiudhuru nafasi yake muda wowote kuanzia sasa

Tayari mataifa mengine mengi katika nchi zilizoendelea tayari yamesema yataanza kufanya uchunguzi kugundua kama kampuni ya Volkswagen ilifanya udanganyifu huo kwenye nchi zao pia. Kosa hili limeiweka kampuni hiyo katika hali ngumu, watachunguzwa na wanaweza kujikuta katika faini za mabilioni ya pesa. Nchini Marekani wanaweza kujikuta wakipigwa faini ya zaidi ya milioni 70 kwa kila gari lililouzika likiwa na teknolojia hiyo ya udanganyifu. Pia makampuni mengine ya magari yatachunguzwa pia kujua kama utumiaji wa teknolojia hizo za udanganyifu zimetumiwa na wao pia.

Uporomokaji wa thamani wa hisa za kampuni hiyo

Uporomokaji wa thamani wa hisa za kampuni hiyo

Kampuni ya VM imekuwa ni moja ya kampuni inayotengeneza faida kubwa sana na kupata sifa nzuri linapokuja suala la ubora wa teknolojia na hivyo skendo hii inategemewa haitaishia kuharibu mtaji wao katika soko la hisa tuu, skendo hii tayari inaharibu sifa ya muda mrefu ya ubora wa magari yake.

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Comments

  1. […] Mwezi Septemba mwaka jana mamlaka za Marekani ziligundua kwamba magari yanayouzwa Marekani ya Volkswageni yalikuwa yanafungwa kifaa fulani ambacho kilikuwa kinatambua gari linapokuwa katika vipimo na kisha kubadili … […]

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania