Kwenye kuchaji simu ni watu wengu wanafanya makosa mbalimbali ambayo yanasababisha mfumo wa kuchati au ata betri za simu zao kuharibika mapema. Leo fahamu mambo ya uzingatia katika kuchaji simu na kufanya betri zidumu.
Fahamu kwa kufuata baadhi ya haya maelezo kutahakikisha betri la simu yako haliwahi kuchoka – hii ikimaanisha uwezo wa kuchaji kwa haraka, na uwezo wa kukaa na chaji kwa muda mrefu.
1. Usiwe unaacha simu yako iishe chaji hadi 0% kila saa

Kuisha kwa chaji hadi mwisho mara kwa mara kunaharibu uwezo wa betri la simu yako kukaa na chaji muda mrefu na pia kunaathiri kasi yake ya kuchaji haraka. Anza kuweka utaratibu wa kuchaji simu yako ikiwa kati ya asilimia 5 – 50%.
2. Kuacha simu yako kwenye chaji muda mrefu
Kuacha simu yako kwenye betri muda mrefu hasa pale ambapo imeshajaa inaharibu ubora wa betri la simu yako. Hii inahusisha wale wenye tabia ya kuweka simu kwenye chaji usiku kucha, kuweka simu kwenye chaji muda wote kazini n.k… hizi zote ni tabia zinazoua ubora wa betri la simu yako.
Kuacha simu ambayo ishajaa kwenye chaji inalazimisha betri kutengeneza joto jingi zaidi ya kawaida na hili linaharibu ubora wake.
3. Utumiaji wa chaja zisizokuwa na ubora
Kama umenunua simu kwa bei ya juu, ni bora pia uhakikishe unatumia chaja zenye kiwango cha juu. Chaja ambazo hazina ubora nje tuu ya kuchaji simu yako kwa utaratabu pia zinaweza kuharibu mfumo wa kuchaji simu yako (charging system).
4. Kuchaji simu yako wakati ina joto kali
Je simu yako ilikuwa eneo lenye joto kali? Iwe uliisahau eneo la dirishani au kwenye gari na matokeo yake simu kuwa ya moto usiiweke kwenye chaji hadi itakapopoa. Kuweka kwenye chaji na kufanya betri kupata umeme wakati lina joto kutasababisha betri kuanza kupoteza ubora wake.
Je ni wapi wewe umekuwa ukikosea zaidi?
Soma pia;
- Utafiti: Hizi ndio Apps zinazokula sana Chaji ya Betri na nafasi katika simu za Android
- Ukiona haya, Fahamu muda wa Kubadilisha Betri la simu yako umefika!