fbpx
Apple, apps, Teknolojia

App ya Siri yakosea; yatoa majibu yasiyosahihi

app-ya-siri-yakosea-yatoa-majibu-yasiyosahihi
Sambaza

Ni ngumu kuamini kuwa kompyuta nayo inaweza kukosea wakati fulani kwani wengi wetu tunaamini kuwa kompyuta ni “Ubongo wenye akili isiyokosea”.

Si sawa kuziamini kompyuta zetu kwa asilimia zote kwani ni dhahiri kuwa kompyuta nayo inaweza ikakosea kwa kutoa jibu lisilosahihi/kufanya kitu tofauti na ilivyoamriwa. Kujua zaidi kuhusu app ya siri ingia-> hapa kupata kuijua app ijulikanayo kama Siri iliyo chini ya kampuni nguli-Apple.

INAYOHUSIANA  Utafiti: iPhone ni za wanawake masikini, Huawei ni kwa wanaume wenye nazo!

siri iphone simu

Majibu yenye utata kutoka kwa app ya siri
Majibu yenye utata kutoka kwa app ya siri

Kukosea kwa app ya app kumejiri baada ya kuulizwa tarehe ya mwisho ya wamarekani kujisajili katika daftari la wapiga kura na app hiyo kujibu kuwa tarehe ya mwisho ya kusajili watu kwa ajili ya uchaguzi imeshapita ilihali tarehe hiyo bado haijapita ila kila jibo ina tarehe tofauti ya kusajili wananchi wake kwa ajili ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi November.

Ili mwananchi wa Marekani (mwenye haki ya kupiga kura) aweze kupiga kura Nov 8 itambidi awe amesajiliwa. Baadhi ya majimbo nchini humo yanaruhusu mtu kujisajili mtandaoni (online).

Mwezi June Apple walitangaza kuwa app hiyo itakuwa kwenye kompyuta aina ya Mac ambazo zinatengenezwa na Apple (kampuni) kitendo ambacho itasaidia watumiaji wa kompyuta aina ya Mac kuiuliza App ya Siri kwa kile wanachokitafuta kwenye kompyuta na kutoa jibu.

INAYOHUSIANA  Fahamu nini maana ya APK kwenye Android! #Maujanja
Moja ya majibu yayiyosahihi kutoka kwa Siri (app)
Kukosea kwa Siri ni hasara kwa mtumiaji. Moja ya majibu yayiyosahihi kutoka kwa Siri (app)

Hivi karibu app hiyo ilipouliizwa inajisikiaje kuwa kwenye Mac ilijibu kuna nafasi ya kutosha ingawa hakuna madirisha pia kuta za zake  sio za aluminium. Jibu hilo si sahihi kulingana na swali lililokuwa limeulizwa.

Tayari Apple wamekwisharekebisha mapungufu mengi kwenye app hiyo lakini yawezekana uaminifu wa app hiyo kwa watumiaji ukapungua na kufanya idadi ya watu wanaoipakuwa app hiyo kushuka kwa kasi sana.

Facebook Comments

Sambaza
2 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

2 Comments

  1. Undani wa namba '108' kwenye app ya Siri #Maujanja - TeknoKona
    March 21, 2017 at 7:05 pm

    […] wale ambao wanatumia iPhone/bidhaa za Apple watakuwa wanafahamu app ya Siri iliyo mahususi kwa kutoa msaada fulani. Kuiamuru programu tumishi ya Siri kupiga namba 108 si kitu […]

  2. Siri: Programu ya Apple yaita ambyulensi kumsaidia mtoto - TeknoKona Teknolojia Tanzania
    October 9, 2017 at 10:10 am

    […] kumsaidia lakini akaiangusha simu hiyo alipowasha taa. Alipiga kelele akiitaka simu hiyo kuamsha programu ya Siri na kuiambia programu hiyo kuita huduma ya dharura (emergence service) huku akianza kumfufua mtoto […]