Simu janja za Sony Xperia zina umaarufu wake kwa miaka mingi tuu ndani na nje ya Afrika na mwaka huu karibu na mwisho wa robo ya pili kwa 2020 wakaona ni vyema wakatoa Xperia 8 Lite.
Rununu ya Sony Xperia 8 Lite inaweza kuonekana inafanana sana na watangulizi wake lakini tofauti ipo tena kutokana na kile ambacho watu wengi wanakitolea macho wanapoenda kununua simu janja. Je, unajua ni kitu gani?. Pata kufahamu undani wa Sony Xperia 8 Lite kuweza kujua jibu la swali hilo.
Muonekano/Kipuri mama
Simu ya inchi 6, kioo cha LCD, ung’avu wa picha ni wa hali ya juu, inayoendeshwa na Snapdragon 630 inafanishwa sana na Xperia 10 iliyotoka mwezi Februari 2019.
Kamera
Ukiitazama simu hii ndio utaweza kupata tofauti yake na hizo nyingine inazofanana nazo. Nyuma ina kamera mbili; ile kubwa ina MP 12 na nyingine imepewa MP 8 bila kusahau taa ya mwangaza. Kamera ya mbele ina MP 8 pia Pia, simu husika ina uwezo wa kukuza picha mara mbili zaidi.
Diski uhifadhi/mengiyo
Memori yake ni GB 64 (unaweza kuweka diski uhifadhi ya ziada), RAM GB 4, betri n i2870mAh (inakubali teknolojia ya kuchaji haraka), ina sehemu ya kuchomeka spika za masikioni ukubwa wa mm 3.5, inatumia USB-C, imewekwa Android Pie, inatumia Bluetooth 5.0, rangi ni Nyeupe na Nyeusi na inauzwa $235|zaidi ya Tsh. 540,500 (bei ya kuagiza).
Hao ndio Sony ambao wametoa pacha wa Xperia 10 na kuitofautisha kwenye kamera tu lakini vitu vingine vyote ni sawa na ipo sokoni tangu Septemba Mosi.
Vyanzo: GSMArena, MySmartPrice
Naomba muifafanue simu rununu aina ya oppo find x2 pro
Sawa, tutaichambua.
Naomba kujua ni namna gani unaweza kuondoa mlio unapopita picha kuwa silence?
Weka simu kwenye silence/mute, pia unaweza kuangalia settings/mipangilio ya kamera yako. Kuna sehemu ya kuzima, shuttersound.