Kwa upande mwingine kosa linaweza likaonekana ni dogo na jamaa amechukua maamuzi makubwa na ya hasira sana.
Jamaa huyu ni wa huko nchini ufaransa na sababu ya yeye kuvunja vunja baadhi ya iphone na mac katika Stoo ya kuuza vifaa vya Apple (Apple Store) inahusisha swala zima la malipo yanayotokana na warantii.
Katika video fupi inaonyesha kijana huyo amevunja angalau iphone 12, iMac 4 na MacBook Air moja, hapo usitake kuniuliza hiyo ni hasara kubwa kiasi gani. Na hii ni kwa zile ambazo zilirekodiwa, kama kuna tokeo lilitokea kabla ya watu hawajaanza kumrekodi ni hasara kubwa zaidi.
Leo siongei sana, angalia video ujionee mwenyewe

Ooooh! Ndio lugha ni kifarasa, pole!
Askari ambao wapo katika Mall hiyo walifanikiwa kumshikilia jamaa japokuwa alikimbia na wakafanikiwa kumkamata mpaka polisi walivyo wasili.