Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Anga, Ndege, Teknolojia

Mwaka 2017 ulikuwa mwaka salama zaidi kwa safari za anga

mwaka-2017-ulikuwa-mwaka-salama-zaidi-kwa-safari-za-anga

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

Data mbalimbali zinaonesha ya kwamba mwaka 2017 ulikuwa mwaka salama zaidi kwa safari za anga duniani kote.

Data kutoka kampauni inayojihusisha na masuala ya safari za anga ya To70 pamoja na ripoti ya shirika la masuala ya anga – Aviation Safety Network, zote zinaonesha mwaka 2017 ndio ulikuwa ni mwaka salama zaidi katika historia ya data za usafiri wa anga.

INAYOHUSIANA  Huduma ya Netflix yazuiliwa nchini Indonesia
mwaka 2017 ulikuwa mwaka salama zaidi kwa safari za anga
Mwaka 2017 ulikuwa mwaka salama zaidi kwa safari za anga

Data za To70 zinaonesha ni ajali 0.06 tu zilijitokeza kwa kila safari milioni moja za ndege. Data hizi kwa wastani zinaonesha kwa wastani, ni ajali moja ya kuua ilijitokeza kwa kila safari milioni 16 za ndege.

Data za shirika la Aviation Safety Network zinaonesha ya kwamba ni takribani watu 79 tuu walifariki mwaka jana kutokana na ajali za ndege za abiria. Mwaka 2016 ni watu 303 walipoteza uhai wao katika ajali 16 kama hizo.

*Data hizi hazijahusisha ajali zinazohusishwa na safari za ndege za abiria, na za kijeshi.

Data zinaonesha kushuka kwa ajali zinazosababisha maisha mengi ya watu kupotea kutakuwa kumesababishwa na ukuaji wa teknolojia bora za uhakikia ubora wa mitambo ya ndege kabla ya kuanza kwa safari.

INAYOHUSIANA  Ripoti: Biashara ya mtandaoni yaongezeka kwa wananchi wa Kenya

Kumbuka data zinazohusisha ajali za ndege na vifo vyake zilizoanza kurekodiwa mwaka 1946.

Je, umeshawahi kutumia usafiri wa ndege? Una maoni gani juu ya usalama wa vyombo vya usafiri wa anga ukilinganisha na vya barabara – kama mabasi, n.k?

Vyanzo: BBC, newsreporter.in

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: , ,

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |