fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Kompyuta Microsoft Teknolojia Windows 10

Windows 10 Technical Preview iko Tayari Kupakuliwa

Windows 10 Technical Preview iko Tayari Kupakuliwa

Spread the love
php9agkgh

Muonekano wa ‘desktop’ ya Windows 10 Technical Preview

Siku si nyingi tangu Microsoft walipotangaza toleo jipya la Windows ambalo litaitwa Windows 10 na hivi sasa unaweza kushusha na kupakia toleo la kiufundi zaidi (Technical Preview) kwa ajili ya kushirikiana na Microsoft kwenye mchakato wa kutengeneza Windows hii mpya.

Toleo hili la Windows ni kwa ajili ya watu wenye ujuzi wa ndani kuhusu mifumo-endeshaji ya Windows na wataalamu wa kompyuta na teknohama. Microsoft wanakushauri sana kama we ni mtumiaji wa kawaida na si fundi sana katika masuala ya teknolojia na hasaa teknolojia ya Windows usishushe na kuipakua Windows 10 Technical Preview kwa sababu haipo tayari kwa watumaiji wa kawaida na itakuletea shida sana kiasi kwamba unaweza ukapoteza data zako za msingi.

Microsoft inategemea kwamba kwa kutoa toleo hili la Windows, wataweza kupata mrudisho wa taarifa za kutosha ili kuifanya Windows inayokuja kuwa Windows bora zaidi haijawahi kutokea.
Kama umezingatia tahadhari za Microsoft na bado unatamaani kushiriki katika zoezi hili na hauogopi kupata misukosko, basi unaweza kuangalia video hii ya Windows 10 Tech Preview kujua yale utakayopata kisha ufanye yafuatayo:
1. Fanya ‘Back-up’ ya kompyuta yako kwa kila kitu kilichomo. Kupakia Windows mpya ni kitu ‘serious’ sana.
2. Pata akaunti ya Microsoft kama hauna na hakikisha huduma ya intaneti ya kutosha.
3. Jiunge na ‘Windows Insider Program’ ili kujiunga na jopo la watu wanaoshiriki kuiboresha Windows dunia nzima
4. Hakikisha kompyuta yako ina sifa zifuatazo au juu: Prosesa ya 1GHz, RAM ya GB 1, 32-bit au GB 2 kwa 64-bit, Hard disk ya GB 16, Graphics card ya DirectX 9 na WDDM driver
5. Shusha Windows 10 Technical Preview moja-kwa-moja kati ya hizi:

  1. Ukimaliza kushusha, unaweza kutumia programu yoyote ya kupakia ‘image’ kwenye diski au DVD.
  2. Tumia setup.exe na fuata maelekezo unayopewa kwenye skrini. Ukiulizwa kuhusu ‘product key,’ tumia NKJFK-GPHP7-G8C3J-P6JXR-HQRJR
SOMA PIA  Google Wabadili Uamuzi Kuhusu Blog za Ngono

Kama umejaribu kufanya set-up na ikakataa, usifadhaike wala usishangae kuona kuwa Windows hiyo haipakii kwenye kompyuta yako, inawezekana kuwa prosesa yake bado haijaruhusiwa kutumika na preview hii.

Mambo ya kutegemea na taarifa zaidi:
Kwa hiyo basi, umejikubali kuwa wewe ni fundi wa mambo ya Windows na umeshashusha na kuipakia Windows Technical Preview kwenye kompyuta yako, kuna mambo inabidi uweke maanani:
Kwanza, Microsoft wametoa notisi kwamba hautaweza kucheza DVD kwa Windows Media Player baada ya kupakia ‘preview’ yao.

SOMA PIA  Expiry Date? - Apple: Simu mpya ya iPhone inatakiwa kutumika kwa miaka 3

Pili, kuwa tayari kupata masasisho (‘updates’) lukuki kutoka kwa Microsoft na utaweza kuchungulia program ya mrudisho kutoka kwao (Windows Feedback app) abayo itawatumia Microsoft taarifa mbalimbali kuhusu matumizi yako ya Windows ili kuiboresha zaidi.

Pamoja na mambo kadhaa mapya utayoweza kufurahia na Windows hii mpya, itakuwa vyema kama utaiweka kwenye kompyuta yako ya mbadala baadala ya ile unayoifanyia kazi muhimu kwani haijajulikana bado kuwa itaifanyia nini kompyuta yako, kitu ambacho hutokea mara nyingi kwa programu ambazo ziko bado kwenye majaribio.

Tunategemea kuwa tumekupatia taarifa muhimu kama ulikuwa na shauku la kujaribu Windows 10 mapema, unaweza pia kupata habari nyingi zaidi kuhusu sifa za hii Windows mpya kupitia makala hii.

Picha na vyanzo:

Pocket-lint.com,windows.com, ndtv.com

ecay

Ninafuatilia teknolojia kila siku na ninapenda kutoa ujuzi wangu kuhusu teknolojia. Karibu tuzungumze kuhusu teknolojia hapa teknokona!

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania