fbpx
Chrome, Google, Google Chrome, Intaneti, Kompyuta, Teknolojia, Windows, Windows XP

Mwisho Wa Google Kusasisha (update) Chrome Inayotumika Kwenye Windows XP Waja!

mwisho-wa-google-kusasisha-update-chrome-inayotumika-kwenye-windows-xp-waja
Sambaza

Google imetoa taarifa kuwa inaongeza muda wa kutoa maboresho mabalimbali kwa kivinjari chake cha Google Chrome kinachotumika katika programu endeshaji ya muda mrefu ya Windows XP. Maboresho hayo ni hadi mwishoni mwa mwaka huu tuu.

Taarifa hiyo inamaanisha kuwa Google watajikita tuu katika kutoa maboresho na ubora wa kiusalama katika kivinjari chao kwa miezi 8 zaidi kwa watumiaji wa Windows XP.

Google hapo mwanzo (2013) walisema kuwa  wataacha kuboresha na kuongeza usalama katika kivinjari chao cha Chrome kwa programu-endeshaji ya Windows XP kufikia mwezi wa nne mwaka huu. Lakini taarifa mpya imetoka na inasema kuwa kampuni imeongeza muda kidogo hadi mwishoni mwa mwezi 2015

INAYOHUSIANA  Jinsi Ya Ku'Log Out' Instagram Kwa Kutumia Kifaa Kingine!

April 8, 2014, yaani mwaka mmoja uliopita ndio tarehe rasmi ambayo kampuni ya Microsoft iliachana na kutoa sapoti ya kimtandao, ya kimaboresho na ulinzi kwa programu endeshaji hii na wakaimiza watumiaji wote wahamie kwenye matoleo mapya kama vile Windows 7 na 8.

Kupitia blogu yao ya masuala ya ulinzi, afisa wao Bwana Mark Larson alieleza kuwa kutokana na kukosekana kwa maboresho ya usalama (security Updates) katika kompyuta zinazotumia Windows Xp zaidi ya mwaka mzima sasa, kompyuta hizi zipo katika hali tete na ambayo inaweza leta maafa makubwa sana kwa watumiaji wake kiusalama. Kwa kuwa Chrone inajikita zaidi katika kuhakikisha mtumiaji anatumia intaneti kwa kiwango cha juu chenye usalama ndani yake, kompyuta ambazo hazitumii programu-endeshaji ambazo zinapata maboresho ya kiusalama hazifai kwa sasa kwa kuwa ni rahisi sana kushambuliwa na virusi na hata ‘Malware’.

INAYOHUSIANA  VW yajipanga kuhamia katika utengenezaji wa magari yanayotumia umeme

maxresdefault

“Mamilioni ya watu bado wanatumia kompyuta zenye Windows XP kila siku. Tunataka hao watu wawe na chaguo la kutumia kivinjara kinachoenda na wakati na pia chenye usalama zaidi” – Alisema Mark Larson

Ukweli ni kwamba watumiaji wa Windows Xp ni wengi sana na inawabidi wabadilishe programu-endeshaji hiyo kwa kuwa ina tuhuma za kuwa rahisi kukumbwa na majanga kama yale ya kupata Virus kwa haraka.

Kulingana na taarifa zilizokusanywa na Net Applications, Windows Xp bado ni moja ya programu endeshaji inayotumika zaidi, inashikilia asilimia 16 kwa utumiaji duniani kote kwa data za mwezi uliopita, na hiyo ni namba kubwa kwa Programu-endeshaji ya mwaka 2001. Watumiaji wa Windows Xp wanaweza kupakua kivinjari cha Internet Explorer  hadi toleo namba 8 wakati sasa kuna hadi Internet Explorer 11 ambayo inatumiwa na windows 8.

INAYOHUSIANA  Uber imetoa taarifa za watu millioni 12.

Hali hii imewafanya watumiaji wa Windows Xp kutumia vivinjari vya makampuni mengine kama vile Mozila Firefox na Google Chrome. Lakini kwa kutokana na tamko hili kutoka Google inategemewa itasaidia katika kuwafanya watumiaji wa programu endeshaji hii kuhamia kwenye Windows 7 au mengine hivi karibuni.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Hashdough

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Reply your comment

Your email address will not be published. Required fields are marked*