fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Kompyuta Teknolojia

Tarehe ya Kuja Windows 10 Yafahamika!

Tarehe ya Kuja Windows 10 Yafahamika!

Spread the love

Wengi wetu tumekuwa tunasubiria kwa hamu kuja kwa Windows 10, na baada ya Microsoft kuficha tarehe rasmi kwa muda mrefu mmoja wa washirika (partner) wake wa muda mrefu kibiashara ametoa siri hiyo kwenye akiwa kwenye kikao muhimu. Na kwa kifupi inakuja mwezi wa 7 mwaka huu.

Microsoft_2014_windows10Tayari Microsoft ilishasema toleo hilo linakuja mwaka huu ila ilikuwa bado haijafahamika ni mwezi gani hasa programu endeshaji hii mpya itaweza kupatikana kwa watumiaji wote. Akiwa katika kikao cha mfumo wa simu (conference call) na wadau wa kampuni ya AMD, mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo Bi Lisa Su alijikuta akitamka ya kwamba toleo hilo la Windows 10 litatolewa mwishoni mwa mwezi wa saba.

SOMA PIA  App Zitakazowapa WanaDSM Anuani kwenye Ramani

[AMD ni kampuni kubwa inayotengeneza vifaa muhimu vya ndani vya kompyuta kama vile CPU na kadi-muonekano (graphic cards)]

‘Mwishoni wa mwezi wa Saba’ – Tegemea kuweza kuipata Windows 10

Toleo la Windows 10 ni tegemeo kubwa kwa kampuni ya Microsoft katika kukuza mauzo yao. Kwani toleo la Windows 7 halikupata mafanikio waliyokuwa wanayataka na wakajikita kutengeneza Windows 8 ambayo ilikuja na mabadiliko mengi sana… nayo haikufanya vizuri kwani ata wale wachache waliohama kutumia Windows XP waliona ni bora kuhamia Windows 7 kuliko 8. Na hadi sasa bado Windows XP ambayo ni ya zamani sana (iliingia sooni takribani miaka 13 iliyopita) inashika namba mbili katika utumiaji baada ya Windows 7 huku Windows 8 ikishika namba 3.

Soma Pia

Je na wewe unasubiria kwa hamu toleo hili la Windows? Unadhani Windows 10 itafanya vizuri zaidi ya Windows 7 na 8?

SOMA PIA  PowerAmp 3.0 : App bora ya kusikilizia mziki yazidi kung'aa

Endelea kutembelea mtandao namba moja wa habari na maujanja ya kiteknolojia Tanzania.

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania