Bill Gates ni mwekezaji wa marekani, Programa wa kompyuta, Mwekezaji na mwenyekiti wa zamani wa Microsoft (Kampuni kubwa ya programu duniani). Tangu mwaka 1995 amekua namba moja katika orodha ya matajiri wakuu (forbes) duniani isipokua mwaka 2008 ambapo alikua namba 3. Unaweza usijue lakini kila sekunde Bill Gates anainginza takribani dola 250 za kimarekani, Na kwa dakika nzima anaingiza takribani dola 15000. Unashangaa??. Kwa kukushangaza zaidi, endelea kusoma mambo 16 ya ukweli wa kuvutia kuhusu Bill Gates
- Bill Gate alianza kuandika program za kompyuta alivyokua na umri mdogo (miaka 13). na programu yake ya kwanza ilikua ni game ya ‘tic tac toe’ amabayo mchezaji alikua anacheza na kompyuta
- Alijua atakua milionea siku moja. Hii ilimpelekea mpaka kujisifia mbele ya mwalimu wake. Bill Gates alitabiri atakua milionea akiwa na miaka 30 lakini akawa bilionea akiwa na miaka 31.
- Aliuza ‘software’ yake ya kwanza akiwa na miaka 17 kwa dola 4200 za kimarekani kwa shule ya sekondari na ilikua ni ratiba ya shule.
- Alishinda maksi 1590 kati ya 1600 kwenye SAT (Scholastic Aptitude Test). Matokea hayo ya 1590 yalikua yanajumuisha IQ ambayo alikua na alama 170. Baadae kulingana na matokeo yake, chuo kikuu cha Havard kilimsajili.
- Bill Gates ni mmoja kati ya wale walioacha shule! Aliacha chuo katika miaka yake ya mwisho. Hata hivyo mwaka 2007 alipata Degree yake kutoka Havard. Hii ni pale Chuo cha Havard kilipompa Degree ya kuheshimiwa kwa mambo alioyafanya.
- Aligundua Microsoft katika umri wa miaka 20, yeye na Paul Allen mnamo Aprili 4, mwaka 1975. Mpaka sasa Microsoft ndio kampuni kubwa ya software duniani
- Mmoja kati ya wakubwa wa kampuni alisema baada ya kumuonyesha gemu Bill Gates na kumfunga kwa pointi 37 na Bill akiwa na pointi 35. Alivyokutana nae mwezi uliofuata, Bill alishinda au kutoa Dro kwa michezo yote waliocheza kwenye gemu hiyo hiyo. Katika huo mwezi mmoja aliisoma hiyo gemu.
- Bill Gates alitangaza kuwa hatawaachia wanawe utajiri wake ila atawapatia kila mmoja dola milioni 10 za kimarekani (watoto wapo wa 3) kati ya utajiri wake wa dola bilioni 72 za kimarekani.
- Tangu Mwaka 1995 amekua namba moja katika orodha ya matajiri wakuu (forbes) duniani isipokua mwaka 2008 ambapo alikua namba 3 akiwa na utajiri wa takribani dola bilioni 58 za kimarekani. Mwaka huo Bw. Warren Buffet ndio alikua mtu namba mmoja akiwa na utajiri takribani dola za kimarekani bilioni 62 akifuatiwa na Bw.Carlos Slim akiwa na utajiri wa takribani dola bilioni 60 za kimarekani
- Kama Bill Gates angekua ni nchi, basi angekua ni nchi ya 37 kwa utajiri duniani!
- Bill Gates anaweza akagawa Dola 15 za kimarekani kwa kila mtu duniani na bado akabakiwa na dola milioni 5 za kimarekani mfukoni.
- Kama akiangusha dola 1000 za kimarekani hana haja ya kuziokota kwa sababu ndani ya sekunde 4 ambazo angeweza kuziokota angekua tayari ameshazirudisha.
- Kama ukizibadili (change) hela za Bill kuwa katika noti ya dola 1 ya kimarekani utaweza kutengeneza bara bara ya kutoka duniani hadi mwezini mara 14 kwenda na kurudi.
- Gates ameokoa maisha zaidi ya milioni 5 kwa kuchangia zaidi ya nusu ya utajiri wake kwenye chanjo na sehemu zinazohusika na afya za watoto.
- Bill ana miaka 40 sasa. Tukichukulia kwamba ataishi miaka 35 zaidi, itamlazimu kutumia japo dola milioni 6.78 za kimarekani kwa siku ili amalize hela zake zote kabla hajaenda peponi (ha!)
- Ukiachana na kompyuta, pia Bill Gates ni muandishi. Mpaka sasa ana vitabu viwili amabavyo ni ”The Road Ahead'” na ‘Business at the Speed of Thought’.
Je unafahamu kingine ambacho hakipo hapa? Tuambie.
nimeipenda hivyo maana ni mungu ndio anapanga na yeye ndio ameamua nani awe mbele na nani afuate big up yaani kama sindano mbele kamba nyuma