fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Picha Snapchat Teknolojia

Miwani janja toleo la pili kutoka Snapchat

Miwani janja toleo la pili kutoka Snapchat

Spread the love

Mbali na kwamba wanafahamika kwa kuwa na programu tumishi inayolenga uchapishaji wa picha/picha mnato lakini pia Snapchat wana bidhaa nyingine (miwani janja) na zimekuwa zikifanya vyema tangu kuzinduliwa kwake.

Snapchat wamezindua toleo la pili upande wa miwani janja ambapo bidhaa hizo zipo mbili, Veronica na Nico. Kiumuonekano ni miwani kama zilivyo nyingine lakini zinajitofautitisha na nyinginezo kwa teknolojia iliyowekwa huko.

SOMA PIA  Gemu ya mpira kwenye app ya Facebook Messenger

Bidhaa hizo zina sifa zote ilizonazo toleo lililopita lakini kuna maboresho madogo ambayo yamefanya kwenye toleo la sasa nilimaanisha ubora wa kurekodi picha mnato kwa kutumia muwani hizo.

Miwani janja

Miwani janja toleo la pili kutoka Snapchat inayofahamika kama Nico. Toleo la kwanza kwa bidhaa hizo lilitoka mwezi Aprili 2018.

Tofauti nyingine ambayo mtu ataiona kwenye miwani janja za Nico na Veronica ni lenzi zake kuwa katika muundo ambao hivi sasa unakuwa ukitoa picha ambayo imelenga eneo husika.

Tangu kuja kwa vitu hivyo walete miwani janja machapisho ya picha/picha mnato yameongezeka kwa 40% kwenye Snapchat ambapo mtu anakuwa ametumia bidhaa hiyo kuweza kupiga picha.

Miwani janja

Toleo la hivi sasa linakuja na mfuko wa kuhifadhia wenye rangi Nyeusi.

Unataka kujua bei? Miwani hizo zinauzwa kwa $200|Tsh. 460,000 ukiagiza na tayari zimeshaanza kuuzwa zikiwa zimeboreshwa njia rahisi za kuweza kuzirusha kwenye mitandao mingine ya kijamii.

Vyanzo: The Verge, CNET, TechCrunch

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Comments

  1. […] post Miwani janja toleo la pili kutoka Snapchat appeared first on TeknoKona Teknolojia […]

TeknoKona Teknolojia Tanzania