Ripoti iliyotolewa hivi karibuni inasema Kampuni ya Samsung inatarajia kusambaza na kuuza simu janja milioni 320 kwa mwaka 2018 duniani kote.
Katika taarifa hiyo pia inatarajia kuuza simu za kawaida (feature phones) milioni 40, tabiti milioni 20 na vifaa vingine vya simu milioni 5. Mauzo ya simu za Samsung Galaxy yamekuwa yakipanda mwaka hadi mwaka kutokana na uzuri na ubora wa simu zinazozalishwa na kampuni hiyo.
Malengo ya Samsung ya wingi wa uuzaji simu zake kwa mwaka huu (2018) ni tofauti na washindani wake wa karibu wa Apple na Huawei. Apple inatarajia kuuza simu zake milioni 200 kwa mwaka 2018 na Huawei inataraji kuuza milioni 150.