fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

apps instagram Intaneti

Akaunti zinazotukana wanamichezo kufungiwa Instagram

Akaunti zinazotukana wanamichezo kufungiwa Instagram

Spread the love

Akaunti zinazotukana wanamichezo kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram kuchukuliwa hatua hii ikiwa ni pamoja na kufungiwa.

Baada ya malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wanamichezo na vyombo vinavyowawakilisha, kampuni ya Facebook – ambao ni wamiliki wa mtandao wa kijamii wa Instagram wasema wataanza kuchukua hatua kali dhidi ya akaunti zinazotumia mtandao huo wa kijamaa kutukana wanamichezo.

Akaunti zinazotukana wanamichezo

Akaunti zinazotukana wanamichezo kufungiwa Instagram: Anthony Martial (kushoto) na Marcus Rashford ni baadhi ya wachezaji waliotukanwa sana kwenye mitandao ya kijamii

 

SOMA PIA  Google kuwezesha mtu kuweka taarifa binafsi mtandaoni

Katika mabadiliko ya sheria au mikataba ya watumiaji wa mtandao huo wa kijamii, Facebook wamesema akaunti zitakazoripotiwa kutuma ujumbe (DM) wa matusi kwa akaunti za wanamichezo zinaweza jikuta kufungiwa kabisa kutoka kwenye huduma ya Instagram.

Katika wiki chache za hivi karibuni wachezaji kama vile Marcus Rashford na Axel Tuanzebe wa Manchester United wamelalamika juu ya kutukanwwa matusi ya kiubaguzi kupitia mtandao huu wa kijamii. Inadaiwa wengi wanapata shida zaidi pale matusi hayo yakitumwa kwa njia za ujumbe wa DM – na sasa Facebook moja kwa moja watachukua hatua kali kwa mtu yeyote ambaye akaunti yake itaripotiwa kutuma ujumbe wa matusi.

SOMA PIA  Watafiti wa MIT - Ufunguaji wa Mitandao (tovuti) Kuwa Kasi kwa Zaidi ya 34%

Wengi wana mtazamo jambo hili litasaidia sana katika kupunguza tatizo hili ambalo limewafanya hadi baadhi ya wanamichezo kuacha kutumia akaunti zao moja kwa moja, na kuwaachia kazi hiyo watu spesheli kwa usimamiaji wa akaunti za mitandao ya kijamii.

Vyanzo: SkySports na Facebook
Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania