Ushawahi tafuta sababu kwa nini usitumie Windows 7 kwenye kompyuta yako? Basi FBI wanakupa sababu.
Shirika la Upelelezi la Marekani, FBI, limetoa tamko likisema usitumie programu ya TeamViewer wala programu endeshaji ya Windows 7 kama una mambo ambayo utaki yaweze kufikiwa na wadukuzi.
Ujumbe wa FBI ulitoka Jumanne hii ukisihi makampuni binafsi na yale ya umma kuchukua hatua dhidi ya nywila (passwords) zisizokuwa imara, programu endeshaji ya Windows 7 pamoja na programu ya kuwezesha utumiaji kutoka mbali – TeamViewer.
1. TeamViewer
Programu ya TeamViewer inawezesha mtu yeyote aliyembali na kompyuta nyingine kupata kuweza kuingia, kupitia nywila spesheli, na kuiendesha kompyuta iliyombali naye. FBI wanasema udukuzi uliotokea siku chache zilizopita katika kituo cha usimamiaji wa mitambo ya maji safi ulihusisha mdukuzi kudukua programu hiyo.
Siku chache zilizopita tuliandika kuhusu udukuzi wa kituo cha usimamizi wa maji safi ya jiji moja Marekani, ambapo mdukuzi alitaka kuongeza kiwango cha kemikali ili kufanya maji hayo kuwa hatari kwa afya za yeyote ambaye angeyatumia. FBI wamesema uchunguzi wa haraka unaonesha mitambo hiyo ilikuwa inatumia programu ya TrueViewer pamoja na programu endeshaji ya Windows 7, vitu ambavyo kwa pamoja wameona vitakuwa vimechangia katika udukuzi.
2. Programu Endeshaji ya Windows 7
Pia FBI wameshauri makampuni na mashirika ya umma kuacha kutumia programu endeshaji ya Windows 7. Mifumo ya kompyuta iliyokuwa inatumika katika kituo hichi cha undeshaji mifumo ya maji safi ya jiji ilikuwa inatumia programu endeshaji ya Windows 7. FBI inakumbusha watu na mashirika ya kwamba programu endeshaji hii haipati masasisho (updates) ya usalama tena. Suala linafanya iwe rahisi wadukuzu kudukua kompyuta yoyote inayotumia programu endeshaji hii.
Microsoft na ata FBI wanashauri watu wawe wanatumia programu endeshaji ya Windows 10.
FBI bado wanashauri mashirika na makampuni kuchukua hatua zote za kiusalama wa data kama wanavyoshauri. Hii ni pamoja na utumiaji wa nywila zilizongumu kugundulika na kuhakikisha wanatumia programu endeshaji ya kisasa na programu za usalama dhidi ya virusi vya kidigitali (antivirus).
Chanzo:
No Comment! Be the first one.