‘Mouse’ ni kitu cha msingi sana katika Kompyuta, lakini kazi nyingi za kompyuta hata simu janja zinafanya siku hizi. Kama kawaida yetu TeknoKona huwa tunakuletea habari na maujanja mbalimbali ya teknolojia, na leo tunakuja na Remote Mouse.
Hivi ni mara ngapi umekuwa unataka kutumia kompyuta yako bila bugudha na ukashinda? Fikiria ukitaka tumia kompyuta ukiwa kitandani! 😆 … Simu yako inaweza ikawa ndio suluhisho la hilo jambo.
Programu tumishi: Remote Mouse
App ambayo tunakuwekea mezani leo ni App inayojulikana kama Remote Mouse, ili kuifanya ifanye kazi fuatilia maelekezo haya:-
- Ishushe Hapa PlayStore|AppStore kupitia simu janja yako au tabiti.
- Ukishamaliza, sasa nenda kashushe ‘Remote Mouse‘ katika Kompyuta yako. Kufanya hivyo ingia katika mtandao huu na kisha shusha kulingana na aina ya kompyuta ambayo unayotumia.
- Baada ya hapo inakubidi uunganishe kifaa chako (simu/tabiti) na komypyuta kwa kutumia WiFi
- Fungua Remote Mouse katika simu yako na kisha chagua jina la Kompyuta yako katika orodha ya majina ili kuunganishwa.
- Kisha utapata utambulisho mfupi halafu ‘Mouse’ itaonekana na itakuwa tayari kwa kutumia.
Ukiachana na hilo pia programu tumishi husika inaweza ukaitumia kama ‘kicharazio (keyboard) cha kompyuta kabisa kwa kuchagua kialama cha ‘kicharazio, pia njia za mkato kama Windows+R, CTRL+W, ALT+F4, n.k unaweza ukazipata kwa urahisi kabisa ndani ya programu hiyo.