Uwezo wa kurudisha kile kilichokuwa kimehifadhiwa kwenye memori ya simu

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Tatizo ambalo wengi wanakumbananalo ni kitendo cha kufuta vitu kwenye simu ambavyo alivihifadhi kwenye memori ya simu (na ndio mazoea ya wengi) na kujikuta anapoteza vitu mbalimbali kama picha, nyimbo, n.k.

Kama wadau wa teknolojia tumekuwa tukikumbana wa swali hili: “Inawezekana kurudisha vile vitu ambavyo mtu amevifuta vilivyokuwa vimehifadhiwa kwenye memori ya simu?” Kwa kupitia vyanzo mbalimbali imefahamika kuwa ndio, jambo hilo linawezekana.

Ni muhimu kuelewa kuwa ili kuweza kufanikisha vitu kama kurudisha vitu mabalimbali ambavyo kwa namna moja wa nyingine havipo tena kwenye simu (vimefutwa/vimefutika) ni lazima laptop, programu wezeshi (software), simu na USB vitumike vyote kwa pamoja.

INAYOHUSIANA  Maujanja: Jinsi Ya Kumblock Mtu Instagram

Fuata hatua zifuatazo kurudisha vitu ulivyokuwa umevifuta.

Ni lazima programu wezeshi itumike kufanikisha zoezi hili na software ambayo tunashauri kutumia ni Active@ File Recovery sababu ikiwa ni software hii inaweza kurudisha mafaili yaliyokuwa yamefutwa kwenye uhifadhi wa ziada (memori kadi) au kwenye memori ya simu. Sababu ya pili ni kwamba Active@ File Recovery inafanya kazi kwenye matoleo kadha wa kadha ya Android (Jelly Bean, Donut, Honeycomb, Ice Cream Sandwich, n.k).

INAYOHUSIANA  Vodacom Cheka Nao; Sasa Masaa 24!

Pakua: Active@ File Recovery

SOMA PIA: Jinsi ya kurudisha mafaili yaliyojificha

  • Pakua programu wezeshi ijulikanayo kama Active@ Recovery. Fungua programu wezeshi ya Active@ File Recovery lakini ukiwa tayari umekwisha unganisha simu yako kwenye kompyuta kwa kutumia waya wa USB: Settings > Applications > Development > USB Debugging kisha iweke on.

    Ukurasa unaonyesha kuwa Active@ File Rcovery tayari ipo tayari kuanza kutumika.

  • Baada ya kuifungua utaarifiwa uchague mojawapo kati ya chaguzi 2, utachagua Recover deleted files. Simu yako ikishatambulika kwenye kompyuta mchakato utaanza na software itaanza kutafuta (scanning).

    Mchakato wa kurudisha mafaili ukiwa unaendelea.

  • Itatokea orodha ya vtu vilivyopatikana baada ya mchakato wa kutafuta kumalizika na utachagua vitu unavyotaka kuvirudisha (recover) kwenye simu yako.

    Utaweza kuchagua ni wapi unataka vitu vyako vihifadhiwe. Chagua herufi inayowakilisha simu yako.

Active@ File Recovery inafanya kazi kwenye Samsung, LG, HTC, Motorola, Asus, n.k. Tuambie, wewe huwa unatumia programu wezeshi ipi kurudisha mafaili kwenye simu yako?

Vyanzo: file-recovery.com, mitandao mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.