Ni wazi kuwa kama uliingia katika mtandao wa TikTok kwa mara ya kwanza pengine inaweza ikawa ulijutia uchaguzi wa jina la kutumia. Au pengine unahitaji kubadilisha tuu, leo TeknoKona inakuletea hatua za kubadili jina
Mtandao wa TikTok ni moja kati ya mitandao iliyokua kwa kasi na kujipatia umaarufu mkubwa ndani ya kipindi cha muda mfupi sana.
Soma Kila Kitu Kuhusu TikTok Hapa
Ili kuweza kubadilisha jina ingia katika App ya TikTok kupitia kifaa chako kisha katika sehemu ya ‘menu’ ingia katika ‘me’
Profile yako itatokea, ili kutaka kuendelea mpaka eneo la kubadilisha jina ingia katika “Edit Profile”
Ingia katika eneo la username, na kisha hapo unaweza ukabadilisha jina na kuchagua lile ambalo unahitaji. Hapa cha muhimu ni kwa lazima kuhakikisha kuwa vigezo vya kuchagua jina vya TikTok havivunjwi, mfano majina ya matusi n.k
Kingine ni kwamba kama jina limeshachukuliwa basi huna budi kuchagua lingine.. cha muhimu kabisa kingine ni kwamba mtumiaji ana uwezo wa kubadili jina hilo kila baada ya siku 30 hivyo ni muhimu kuwa makini katika kufanya uchaguzi huo.
Ukimaliza tuu kubadili jina hili inabidi uchague neno ‘save’, matokeo yatajitokeza muda huo huo. na mpaka hapo utakuwa umeweza kubadilisha jina lako katika mtandao huo. Hii imekaa poa zaidi kama ulichagua jina ambalo halikuvutii tena.
Niandikie hapo chini katika eneo la comment, hii imekaaje, je wewe ni mtumiaji mzuri wa mtandao huu wa kijamii? Kumbuka Kutembelea Mtandao wako wa TeknoKona kila siku kwani daima tupo na wewe katika teknolojia!.
No Comment! Be the first one.